TREVO:Je ni kweli TREVO Inatibu au ni utapeli?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Habarini wana JF

Kwanza kabisa natambua kuwa Tiba yoyote ile ni imani lakini sio imani tuu lazima na tiba ifanye kaZi

Kwasasa hasa hapa nchini kwetu Tanzania kumekuwa na Tiba asilia nyingi sanaaaa hadi unashindwa kujua ipi ni ipi hasa hii ya watu kujitangazia Tiba zao

Kwasasa TREVO naona inashika kasi sana lakini kiupande wangu nasikia shuhuda tuu toka kwa wauzaji na wahamasishaji wa hii Tiba nashindw kuelewa kama kweli inafnya kazi kama vile navo ambiwa

Nambiwa ni virutubisho na sio dawa lakini shuhuda nazo pata naona watu wanapona magonjwa ambayo ni very very complicated hadi najisemea mwenyewe kama mtu anasimulia kuwa mtu mwenye cancer ambayo ipo stage kubwa kapona sa serikali inasubiri nini kugawa dawa hii kwa wagonjwa

Napata shuhuda za magonjwa makubwa makubwa kabisa na naambiwa kopo moja la TREVO NI laki moja na 80 hadi na 95!

Swali langu ni je kweli hii TREVO inafanya kazi kama vile inavotangazwa au ni propaganda za kumuibia Mtanzania?

Kama kuna mtu hapa alikuwa na mgonjwa wake atwambie kama alipona kwa TREVO

sipo hapa kuwaharibia ila nikutaka kupata ukweli ili tuwasaidie na wengine!
 
Ingia upigwe, ingekuwa inatibu WHO wasingeiacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…