BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Katika ujumbe wa video, alisema "alijawa na shukrani kwa ajili ya safari" lakini kwamba kulikuwa na "sehemu nyingine ya maisha yangu ambayo ninataka kuendelea kuifatilia".
Mchekeshaji huyo mwenye miaka 38 amekuwa kwenye kipindi hicho tangu achukue mikoba ya Jon Stewart mnamo 2015.
Alisema muda wa kuondoka kwake utatangazwa baadaye na kwamba ataendelea kuwepo kwa muda huo huo.
Noah alianza uchekeshaji wake katika nchi yake ya asili ya Afrika Kusini, akitoa safu ya vipindi maalum na kuandaa kipindi cha mazungumzo usiku wa manane kabla ya kuhamia Marekani make 2011.
Bado alikuwa jamaa asiyejulikana alipochaguliwa kuchukua kipindi cha Daily Show kwenye mtandao wa Comedy Central, lakini tangu wakati huo amekuwa nyota anayetambulika kimataifa na kushinda tuzo nyingi za televisheni.
Akitangaza kuondoka kwake, aliwashukuru wafanyakazi na watazamaji wa kipindi hicho kwa "miaka saba ya kushangaza", na kuongeza: "Imekuwa ya kishenzi, ya kishenzi kweli".
“Nakumbuka tulipoanza..., watu wengi sana hawakutuamini,” alisema. "[Kuniteua kama mwenyeji] ilikuwa dau la kichaa kufanya. Bado nadhani lilikuwa chaguo la kichaa, Mwafrika huyu wa kubahatisha.
"Ninajipata tu nikijawa na shukrani kwa ajili ya safari. Imekuwa ya kushangaza kabisa. Ni kitu ambacho sikuwahi kutarajia."