Trial deno ama retrial ni pale kesi inapoamriwa kusikilizwa upya kwakuwa kuna mapungufu makubwa ya kisheria ambayo mahakama yenye mamlaka ya kusikiliza rufaa yaani 'appellate court' imeyaona katika rufaa dhidi ya kesi iliyoamriwa awali na mahaka iliyosikiliza shauri 'trial court'.
Mara nyingi, mahakama inaamuru shauri au kesi isikilizwe upya na hakimu ama jaji mwingine, mazingira ya uamuzi wa trial denovo hutegemea na kesi husika pamoja na utashi wa mahakama ila ni lazima misingi ya haki izingatiwe kabla ya kutoa amri hiyo ya trial denovo.
Res judicata, ni kanuni ktk sheria ya mwenendo wa madai, inayotaka shauri lilosikilizwa na kumalizika mbele ya pande mbili zile zile, suala lile na watu wale wale lisiletwe tena mahakamani kusikilizwa upya.