Tribalism & Nepotism; Uhuru awapa Kazi jamaa zake, wakenya wamjia juu.

Tribalism & Nepotism; Uhuru awapa Kazi jamaa zake, wakenya wamjia juu.

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617
Kama kawa kama dawa, Uhuru Kenyatta ameendeleza ile jadi na utamaduni wa wakenya wa kuendekeza ukabila na upendeleo katika kutoa ajira na nafasi teuzi za serikali.

Huwa ndugu zetu wakenya (wakikuyu na idots), wanasema Uhuru Kenyatta hawezi kumfukuza mtu Kazi kwasababu katiba inamfunga mikono, vipi kuhusu kuteua na kuajiri jamaa zake, katiba inamruhusu?

===

Wazee hujuana: Rais Kenyatta amzawadi mwanawe Maina Kamanda

Rais Uhuru Kenyatta amekashifiwa na baadhi ya Wakenya baada ya kumteua mwanawe Maina Kamanda kwenye Tume ya Kitaifa ya uwiano na utengamano (NCIC).

Kwenye orodha iliyotolewa na Rais Kenyatta, Danvas Makori, ambaye ni mumewe mwanawe Maina Kamanda alitajwa kama mmoja wa walioteuliwa.

Wakenya wamfokea Rais Kenyatta baada ya kumpa kazi mwanawe Maina Kamanda

Wakenya wamemfokea Rais Uhuru Kenyatta baada ya kumteua mwanawe Maina Kamanda kwenye tume ya NCIC. Picha: State House
Source: Facebook

Uteuzi huo ulitangazwa Jumanne, Oktoba 22, huku ikiwa na majina ya Samuel Kobia (72) na pia aliyekuwa mbunge wa Rangwe, Philip Okundi wa miaka 77.
Wakenya hata hivyo walikerwa na kuwepo kwa makori kwani kando na kuwa na mwanawe Kamanda, vile vile alifurushwa kutoka serikali ya kaunti ya Nairobi kwa madai ya kuhusika kwenye ufisadi.

Wakenya wamemfokea Rais Kenyatta baada ya kumpa kazi mwanawe Maina Kamanda, Danvas Makori. Picha: Standard

Source: UGC
Makori alifurushwa na gavana Mike Sonko baada yake kusema waziri huyo alikuwa akihusika katika kuipora serikali ya kaunti hiyo mamilioni ya fedha.
Kando na kero la Wakenya kwa Makori, Rais Kenyatta pia alimteua aliyekuwa mbunge wa Othaya Mary Wambui kwenye tume nyingine licha ya kuwa amewahi kukiri hana masomo ya kutosha.

Hatua hiyo iliwakera sana Wakenya ambao wameuliza maswali ni kwani vijana walio na masomo na kukosa nafasi za kaszi hawapewi nafasi.

Rais Uhuru Kenyatta alimchagua Mary Wambui na kuzua tetesi kali kutoka kwa Wakenya. Picha: Daily Nation
Source: UGC

Uteuzi wa wazee ndani ya serikali ya Rais Kenyatta ulianza wakati ambapo aliyekuwa makamu wa rais Moody Awori alipewa kazi.

Awori ana miaka 92 na kupata kazi kwake serikali kuliwaacha vijana ambao Jubilee iliahidi kuwapa nafasi za kazi wakimeza mate tu.

Katika uchaguzi wake wa 2013, Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto waliahidi vijana kuwa watatoa mabango ya ukosefu wa kazi na kuweka yale ya kutangaza nafasi za kazi.

Huyo ndio kiongozi wa nchi, hapo anatueleza taswira ya wananchi wake anaowaongoza, ni kawaida Kenya hata kuingia chooni vimepagwa kima kabila
 
Wanaomkashifu Rais Uhuru si ni sisi wakenya au kuna wakenya wengine? Wakenya huwa hawabebewi akili zao. Mpwa wa Magufuli alipotuhumiwa kwa matumizi mabaya ya umma hamkuthubutu kupaza sauti. Mbaya zaidi ni kwamba muda mfupi baadaye alimteua nduguye kuwa jaji, kwa jeuri. Alafu hadi leo hii vyeti vya kifaranga wa Jiwe 'Bashite' hamjaziona. Yaani mpo mpo tu, ubavu wa kuwakashifu wakenya kwa kumkashifu rais wao unatoa wapi? Aliyeteuliwa sio ndugu ya rais Uhuru, ni mme wa mtoto wa Maina Kamanda, na wala sio mkikuyu, ni mkisii. Kuwa makini tafadhali.
 
Soma kichwa cha habari vizuri, "Tribalism & Nepotism", Maina ni kabila gani?.
 
Soma kichwa cha habari vizuri, "Tribalism & Nepotism", Maina ni kabila gani?.
Yaani niishie kwenye kichwa cha habari ambacho wewe ndio umeandika? Wakati taarifa inasema wazee hujuana? Alafu boss siku nyingine tafuta habari kutoka vyanzo ambavyo ni vya heshima. Hebu uliza wakenya kuhusu hiyo tuko, utajidharau sana.
 
Wakenya nitawaulizaje?, nije Kenya kukutana na wakenya wote?. Tatizo lenu mnadhani ninyi mlioko hapa JF ndio wakenya pekee, kwamba ninyi mnalosema ndio linawakilisha wakenya wote, wakenya wengine wakitofautiana na ninyi, hao mnawaona sio wakenya kamili, au hawajui kitu.

Ukweli ni kwamba baadhi ya wakenya wamechukizwa na kitendo hicho, hiyo haikulazimishi wewe pia uchukie, unaweza kuungana na Uhuru Kenyatta, hilo sio tatizo kwasababu wewe ni mkikuyu lazima umtetee mkikuyu mwenzako
 
Nyani haoni kundule

Watanzania nitawaulizaje?, nije Tanzania kukutana na watanzania wote?. Tatizo lenu mnadhani ninyi mlioko hapa JF ndio watanzania pekee, kwamba ninyi mnalosema ndio linawakilisha Watanzania wote, watanzania wengine wakitofautiana na ninyi, hao mnawaona sio watanzania kamili, au hawajui kitu.

Ukweli ni kwamba baadhi ya Watanzania wamechukizwa na kitendo hicho, hiyo haikulazimishi wewe pia uchukie, unaweza kuungana na Johnny walker Magufuli, hilo sio tatizo kwasababu wewe ni Mfipa lazima umtetee mfipa mwenzako.

Bure kabisa
 
Back
Top Bottom