Trivia: Asili ya msemo "Shamba la Bibi."

Trivia: Asili ya msemo "Shamba la Bibi."

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Nilikuwa napitia kitabu kimoja cha zamani(Mtawa Maporini-2) na nikakutana na neno Shamba la Bibi(Likimaanisha eneo lililohifadhiwa). Basi ikabidi niingie kwenye "shimo la sungura" ili kutafuta maana yake. Inasemwa kuwa msemo huu ulianza kutumika wakati wa utawala wa Ujerumani. Wajerumani walitenga maeneo ya mapori kama Selous kama maeneo ya mke wa Kaizer(Kaizari) wa Ujerumani kuwinda. Watu hawakuruhusiwa kuwinda, kukata miti, kulima au kufanya shughuli yeyote ndani ya mapori hayo. Basi raia wakaanza kuyaita mapori hayo Shamba la Bibi, wakimaanisha shamba la mke wa Kaizari.

Mwishoni mwishoni mwa utawala wa Uingereza msemo huo uligeuka kumaanisha Shamba la Queen Elizabeth wa Uingereza. Leo hii msemo huu umechange nyuzi 180 na unamaanisha mali ambayo mtu yeyote anaweza kuitumia atakavyo.
 
Back
Top Bottom