Inshu ni kwamba viongozi wetu hawaingii madarakani kuifanyia kazi nchi ila wanafanyia kazi nchi zingine! kama kiongozi anaenda nje kila siku anakutana na hizi vitu, kwa nini hata siku moja akasema ngoja nasi tujaribu hata kuboresha mradi mmoja baada ya mwingine seriously siyo kuachia katibu ambaye naye ni chapombe kweli hata plan hana! Nchi yetu ina vichwa kibao zinafanya kazi nje ya nchi, viongozi wetu hawataki changamoto za kuwalipa mishahara mizuri ili wafanyie kazi nchi yetu! Tuna kila sababu ya kuitwa masikini na tuna kila sababu ya kuitwa matajiri kwani wachina hao hao wanapora mali zetu wanatengeneza vitu vikali ambavyo huwezi kuamini raw material yanatoka Tz.
Kwa ufupi, kufanya mabadiriko Tz ni kujitoa mhanga kama sasa watz wanavyoonekana kutaka kufanya! Human resource ipo ya kutosha lakini management ndo mbovu.