Trump aingiwa na ubaridi. Amtaka Zelensky amuombe radhi hadharani ili arudishe uhusiano na Marekani

Trump aingiwa na ubaridi. Amtaka Zelensky amuombe radhi hadharani ili arudishe uhusiano na Marekani

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amuombe radhi hadharani ndipo atakubali kurudisha upya uhusiano kati ya Marekani na Ukraine baada ya Viongozi hao wawili juzi kuzozana mbele ya Waandishi wa Habari katika Ikulu ya Marekani (White House) kitendo ambacho Trump anaamini Zelensky ameidharau Marekani.

Mtandao wa Bloomberg umeripoti kuwa Afisa mmoja wa Ulaya amevujisha taarifa kuwa baada ya malumbanonya Trump na Zelensky, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer aliwapigia simu Viongozi hao wawili na kuwashawishi warejee mezani kumalizia maongezi lakini Trump alisema anahitaji aombwe radhi hadharani na Zelensky na pia nchi ya Marekani kwa ujumla iombwe radhi kwa kilichotokea.
 
Asemekwanza aombwe radhi kwakosagani, labda kwakutovaa suti[emoji1787].

Yeye ndio amuombe radhi Zelensk na wamarekani kwa kutoa kauli ambazo sio za kiungwana na kuonyesha kutowaheshimu viongozi wenzake hasa Biden na Obama.

Trump na JD wamefanya mambo ya kitoto na walimkosea adabu Zelensk.

Ayataje maneno ama vintendo alivyo fanya Zelensk ambavyo vitamlazimu aombe radhi.

Trump angekuwa smart ange muambia makamuwake JD amuombe radhi Zelensk.



Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Pro-Zelensky! Siyo kwamba Trump ameingia ubaridi kwa mtu mdogo Zele
Staimer alikuwa anajaribu kuwapatanisha Trump na Zele! Ndipo Trump aka demand apology kwanza!
 
Huyu Trump alisema akiingia madarakani ataimaliza vita ndani ya saa 24 tu. Imekuwaje tena mwezi unaisha bado anahangaika na Zelensiky?? Na aombwe msamaha kwa kosa gani?

Wale waandishi badala ya kumuuliza Zelensiky kwanini havai suti walipaswa kumuuliza Trump kwanin vita haijaisha ndani ya saa 24.
 
Umri wa trump sasa ni sawa na huyu akili zake kule USA
IMG_0612.jpeg
 
Trump sidhani kama ni kiongozi sahihi wa marekani ana loop holes nyingi za ubabaifu zinazoleta sintofahamu kibao wamarekani wamebet kwenye kura na mkeka ushachanika tayari.
 
Inabidi Trump aombwe radhi kwakua Mkubwa Huwa hakosei, anateleza tu.

So Trump aliteleza Lakini Zelensky alikosea.
 
Back
Top Bottom