Maamuzi ya Bw. Trump, [the disgraced president of the United States of America.,] kuzuia kutoa ada na mchango wake kwenye shirika la afya duniani ni ya kusikitisha mno.
Madhara yake ni makubwa mno. Na ni wazi kuwa yatasababisha milipuko na kushindikana kuyazuia maradhi mengine mfano polio, ebola, ukimwi, homa ya manjano, dengu, nk. kusambaa duniani.
Matendo haya ya Trump yanafananishwa na maandalizi ya kusababisha vifo kwa maelfu au mamilioni kwenye jamii maskini kabisa duniani hasa Afrika.
Kwa maamuzi haya na mengine, baadhi ya wanausalama wa Marekani wameanza kumwona Trump kama tishio la usalama maisha ya binadamu na hata wamarekani.
Trump anaweza kuwa anatenda haya kwa kufuata ushauri wa wapambe wake wanaomwaminisha kuwa yeye yupo sahihi wakati wote.
Zipo dalili za wazi za kuchokwa kwa Bw. Trump na wamarekani na hata na vyombo vya usalama vya nchi hiyo maarufu duniani.
Sisi huku kwa makapuku tuendelee na maisha yetu ya kimaskini na kumtegemea Mungu. Kama ametupangia maangamizi hata Trump hawezi kutuokoa. Kama ilivyoandikwa "Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu".
Ni hoja tu nawasilisha.