Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 384
- 970
Matokeo ya awali yanaonesha kuwa mgombea wa chama cha Republican Donald Trump amepata kura 198 za wajumbe wa kamati maalum ya uchaguzi nchini Marekani, ambayo inamchagua Rais maarufu kama Electoral College, na mgombea wa chama cha Democratic, Kamala Harris amepata kura 109 za Electoral College.
Trump ameshinda katika majimbo ya Kentucky, Indiana, West Virginia, Florida, Oklahoma, Tennessee, Alabama, South Carolina, Wyoming, South Dakota, Texas, Arkansas, Ohio na Nebraska.
Huku Harris akishinda kwenye majimbo ya Vermont, Maryland, Connecticut, New England, Rhode Island, New York na Delaware, ambako ni nyumbani kwa Rais Joe Biden.
Majimbo mengine aliyoshinda Harris ni Mississippi, Massachusetts, New Jersey, Illinois, ambako ni nyumbani kwa rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama. Jimbo hilo limekuwa likiwachagua wagombea wa Democratic tangu mwaka 1992.
Ushindi wa Trump Florida, ni wa mara ya tatu mfululizo. Mgombea wa urais wa chama cha Democratic hajawahi kushinda kwenye jimbo hilo, tangu Barack Obama aliposhinda mwaka 2012.
Katika matokeo ya kura za wananchi wa kawaida zilizohesabiwa hadi muda huu tunakwenda hewani, Harris kapata kura milioni 21,199,192 ambazo ni sawa na asilimia 46.3, na Trump kura milioni 24,234,518 ambazo ni sawa na asilimia 52.6.
Katika uchaguzi wa maseneta, chama cha Republican kimepata 46 na Democratic 35. Aidha, chama cha Republican kimepata wabunge 73 na Democratic wabunge 40, na kwa upande wa magavana, Republican imepata 23 na Democratic
Matokeo ya urais wa Marekani yanaweza kujulikana punde tu baada ya siku ya uchaguzi, au yanaweza kuchukua wiki kadhaa hadi yatakapothibitishwa.
Akizungumza kabla ya vituo vya kupiga kura kufungwa, Trump aliwatolea wito wafuasi wa Republican kuhakikisha wanapiga kura zao, akiwataka walioko katika foleni waendelee kusubiri hadi watakapopiga kura.
Kwa upande wake Harris alikuwa akiwapigia simu wafuasi wake kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kupiga kura.
Kitisho hicho kilisababisha kufungwa kwa muda kwa vituo vitano vya kupigia kura, ili kuwaruhusu polisi kufanya uchunguzi wa vilipuzi hivyo, ingawa hawakukuta kitu chochote.
Hata hivyo, ubalozi wa Urusi nchini Marekani umekanusha madai kwamba nchi hiyo imeuingilia uchaguzi wa urais nchini Marekani na kuyaita madai hayo kuwa ni ''kashfa ya uwongo''.
Source: DW
Trump ameshinda katika majimbo ya Kentucky, Indiana, West Virginia, Florida, Oklahoma, Tennessee, Alabama, South Carolina, Wyoming, South Dakota, Texas, Arkansas, Ohio na Nebraska.
Huku Harris akishinda kwenye majimbo ya Vermont, Maryland, Connecticut, New England, Rhode Island, New York na Delaware, ambako ni nyumbani kwa Rais Joe Biden.
Majimbo mengine aliyoshinda Harris ni Mississippi, Massachusetts, New Jersey, Illinois, ambako ni nyumbani kwa rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama. Jimbo hilo limekuwa likiwachagua wagombea wa Democratic tangu mwaka 1992.
Ushindi wa Trump Florida, ni wa mara ya tatu mfululizo. Mgombea wa urais wa chama cha Democratic hajawahi kushinda kwenye jimbo hilo, tangu Barack Obama aliposhinda mwaka 2012.
Mshindi anahitaji kupata kura 270
Kila mgombea anahitaji kupata kura 270 za Electoral College kati ya 538 zinazohitajika ili kushinda.Katika matokeo ya kura za wananchi wa kawaida zilizohesabiwa hadi muda huu tunakwenda hewani, Harris kapata kura milioni 21,199,192 ambazo ni sawa na asilimia 46.3, na Trump kura milioni 24,234,518 ambazo ni sawa na asilimia 52.6.
Katika uchaguzi wa maseneta, chama cha Republican kimepata 46 na Democratic 35. Aidha, chama cha Republican kimepata wabunge 73 na Democratic wabunge 40, na kwa upande wa magavana, Republican imepata 23 na Democratic
Matokeo ya urais wa Marekani yanaweza kujulikana punde tu baada ya siku ya uchaguzi, au yanaweza kuchukua wiki kadhaa hadi yatakapothibitishwa.
Akizungumza kabla ya vituo vya kupiga kura kufungwa, Trump aliwatolea wito wafuasi wa Republican kuhakikisha wanapiga kura zao, akiwataka walioko katika foleni waendelee kusubiri hadi watakapopiga kura.
Kwa upande wake Harris alikuwa akiwapigia simu wafuasi wake kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kupiga kura.
Urusi yakanusha madai ya kuingilia uchaguzi wa Marekani
Huku hayo yakijiri, kuliripotiwa kitisho cha mabomu kwenye vituo vya kupigia kura huko Georgia. Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI na polisi wa eneo hilo wamesema kulikuwepo taarifa za vitisho 32 vya mabomu vinavyoonekana kutokea Urusi, ambayo imeshutumiwa na Marekani kwa kujaribu kuuingilia uchaguzi wa urais.Kitisho hicho kilisababisha kufungwa kwa muda kwa vituo vitano vya kupigia kura, ili kuwaruhusu polisi kufanya uchunguzi wa vilipuzi hivyo, ingawa hawakukuta kitu chochote.
Hata hivyo, ubalozi wa Urusi nchini Marekani umekanusha madai kwamba nchi hiyo imeuingilia uchaguzi wa urais nchini Marekani na kuyaita madai hayo kuwa ni ''kashfa ya uwongo''.
Nani kuibuka mshindi?
Source: DW