Mgombea wa kujitegemea katika uchaguzi wa urais Marekani Robert F Kennedy Jr ameungana na mgombea wa chama cha Republican, Donald Trump, jukwaani katika mkutano wa kampeni huko Arizona baada ya kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho na kumuunga mkono rais huyo wa zamani wa Marekani.
Kennedy ni mtoto wa Seneta wa zamani wa Marekani Robert F Kennedy na ni mpwa wa rais wa zamani John F Kennedy, akitokea familia yenye ushawishi mkubwa katika siasa za chama cha Democrats.
Kennedy, mwenye umri wa miaka 70, aliyekuwa mwanachama wa Democrats kwa kipindi kirefu katika maisha yake na anayetokea kwenye familia kubwa ya Kennedy, alisema kwamba maadili yaliyomfanya aondoke kwenye chama hicho sasa yamemshawishi "kujitosa nyuma ya rais Trump na kumuunga mkono".
Hali hiyo imetokea baada ya kuvutiwa na sera za Trump ikiwemo
- Kuwatoa michezoni wachezaji wa kiume waliobadili jinsia
- Kufunga mipaka na kuwafukuza maharamia milioni 20 walioingia nchini awamu hii
- kupunguza kodi
- kufuta masomo ya kufundisha watoto wadogo ngono na kubadili jinsia
- n.k.