Trump apewe nuclear codes

kichakaa man

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Posts
5,500
Reaction score
5,164
juzi karibia siku nzima nilikuwa nimekaa mbele ya televisheni kushuhidia hatua kwa hatua tukio la kihistoria la kuapishwa kwa Rais wa 45 wa Marekani ambaye anakuwa ndiye Rais wa kwanza wa nchi ambaye hana historia ya kuwa mwanasiasa hata kuwa "mwenyekiti wa mtaa" au kutumikia jeshi la Marekani.

Baada ya Rais Donald John Trump kumaliza kutamka maneno 35 ya kiapo cha kushika ofisi ya Urais maneno ambayo yanaishia na sentensi inayosema "... so help me God!" Karibia watu laki tisa waliokusanyika Capitol Hill kushuhudia tukio hili la kihistoria walilipuka kwa shangwe na vifijo kuwa sasa ni rasmi Trump amekuwa Rais.

Lakini binafsi yangu, mara baada ya Trump kumaliza kutamka maneno hayo ya kiapo, wazo moja tu likanipitia kichwani mwangu; "kwahiyo now Trump has the nuclear codes"!!

Katika kipindi chote cha kampeni watu kadhaa wazito akiwemo mama Clinton na hata Rais Obama wamekuwa wakikaririwa wakisema kuwa "Trump hana utashi, busara wala utulivu wa ndani wa kumfanya aaminiwe kupewa 'nuclear codes'".
Maneno hayo yalikuwa yakirudiwa mara kwa mara kiasi kwamba yakawa kama wimbo kwamba "Trump sio mtu wa kuaminika na kuuweka ulimwengu wote rehani kwa kumkabidhi nuclear codes"

Sasa swali la kujiuliza, je hofu hii yote ni kwasababu gani?? Na je, baada ya kuapa ameshapewa hizo 'codes' au bado?? Na je hizo 'codes' ni kitu gani haswa??

Ni kwamba, wakati ambapo jana watu wote akili yao ilikuwa ikisubiria tukio kubwa la kuapishwa kwa Trump na labda wale wenye kupenda kufuatilia habari walifurahia kuangalia jinsi Familia ya Trump ilivyowasili Washington, walivyohudhuria ibada kanisani pale DC, na baadae kujumuika na familia ya Obama kupata kifungua kinywa Whitehouse lakini watu wengi hawafahamu moja ya tukio muhimu zaidi lililofanyika jana ambalo hili haliwezi kurushwa CNN, BBC, Fox au chombo chochote kile cha habari ingawa naamini walikuwa wanajua.

Mnamo majira ya saa tatu asubuhi ndani ya ikulu ya Marekani kilifanyika kikao maalumu amabacho kilihudhuriwa na Rais Barack Obama, Rais Mteule Donald Trump, Makamu wa Rais Joe Biden na Makamu wa Rais Mteule Mike Pence na kikao hiki kilisimamiwa na kamandi maalumu ya jeshi la marekani inayoitwa Strategic Command ambao ndio wanaosimamia sehemu zote za siri zenye kuhifadhi silaha za Nuclear (Strategic Nuclear Arsenal). Pia kikao hiki kilikuwa na muwakilishi wa ofisi ya jeshi ndani ya White House (Whitehouse Military Office).

Kikao hiki kilihusu makabidhiano ya "nuclear codes" kutoka kwa Obama kwenda kwa Trump.

Miaka ya nyuma Rais mpya alikuwa anapewa hizi codes Mara baada ya kuapishwa lakini mwaka 1973 utaratibu huu ukabadilishwa ambapo kabla ya Rais mpya kula kiapo kinafanyika kikao cha siri ambacho Rais Mteule anakabidhiwa nuclear codes.

Swali, je hizi codes ni kitu gani?? Ni kama namba ya mpesa au tigo pesa au atm ambayo unakuwa umeikariri kichwani??

Jibu ni kwamba, hizi tunazozisikia zikizungumzwa kila siku "nuclear codes" ni msululu wa vifaa maalumu vya kijeshi vinavyomuwezesha Rais wa Marekani kutumia uwezo wake kama Amiri Jeshi mkuu kufanya shambulio la kinyuklia pale anapoona inafaa kufanya hivyo.
Na ukisikia wanaongelea "nuclear codes" ni kwamba wanaongelea mkoba maalumu ambao mda wote unakuwa umebebwa na Mwanajeshi wa Marine sehemu yoyote ile ambayo Rais wa Marekani anakuwepo.

Sehemu yoyote ile ambako Rais wa marekani anakuwepo ndani ya nchi yake au nje ya nchi.. Mtaani au whitehouse, yaani popote pale alipo..
Watu wengi huwa wanaelekeza akili yao kushangaa wale 'secret service', but next time jaribu kupepesa macho (hata kama unaangalia kwenye TV) utaona kuna Mwanajeshi amevaa sare za Marine (au mara chache sana anavaa suti) amebeba mkoba mweusi uliotuna. Huu mkoba wenyewe wanauita "The Football" na ndani yake ndimo kuna "nuclear codes" na nyenzo nyingine muhimu za kumuwezesha Rais kufanya shambulio la nyuklia.

Ndani ya huu mkoba unaoitwa "The Football" au kama unavyojulikama kwa jina rasmi la kiofisi "The Presidential Emergency Satchel" kuna vifuatavyo;

- kuna kifaa kinafanana kama na laptop
- kuna simu ya kijeshi ya satelaiti
- kijitabu kama kipeperushi chenye maelezo ya namna ya kutumia vifaa vyote ndani ya The Football
- kuna kijitabu chenye maelezo ya hatua za kijeshi na sehemu za kuzilenga kwa mashambulio (retaliatory options)
- kuna kadi ya pembe nne kama kadi ya benki yenye namba za siri. Hii kadi maarufu inaitwa "The Biscuit".

Sasa ikitokea Rais anataka kutumia nyuklia kushambulia mahali fulani.. Huu mkoba unafunguliwa kisha kitufe maalumu kinabonyezwa ambacho inatuma taarifa maalumu inayoitwa "watch alert" kwenda kwa kamati ya Majemedari wa Vikosi vya majeshi ya Marekani (Joint Chiefs of Staff). Na wao wanamshauri Rais namna bora ya kutekeleza shambulio hilo.

Hapa niseme kwamba huu ushauri wa hawa Joint Chief of Staff ni protokali tu kwani Marekani inao mpango maalumu wa kijeshi unaoonyesha namna ya kufanya shambulizi lolote la nyuklia kutegemea na lengo lolote ambalo Rais atakuwa nalo. Mpango huu unaitwa OPLAN 8010 (zamani ilikuwa inaitwa Single Integrated Operational Plan) ndio hii ipo kwenye kile kijitabu kimoja wapo nilichoeleza hapo juu kuwa kipo ndani ya The Football.

Baada ya hapo The Football inatuma signal kwenda National Military Command Center ambayo itampa Rais 'access' ya mizinga yote ya nyuklia ipatayo 4,500.

Baada ya hapo kwa kutumia kile kifaa kama laptop ndani ya The Football atachagua 'location' anayotaka kuishambulia na kisha ataingiza 'codes' zilizopo kwenye kile kikadi kinachoitwa The Biscuit. Na baada ya hapo, booooommb.!! Shambulio linakuwa limetekelezwa.

Nchi nyingine pia zenye nguvu kubwa za kijeshi kama Urusi na China pia wameiga mfumo huu.

Hiki nilichoeleza ndizo "nuclear codes" ambazo walikuwa wanapiga kelele Trump asipewe. Lakini mpaka hivi tunavyoogea tayari anazo na mwanajeshi wa Marine anambebea huo mkoba kila Trump alipo, kwa sababu yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu kwa sasa.

Mizinga hii 4,500 ya nyuklia ina uwezo wa kuisambaratisha dunia yote kama ikirushwa sehemu tofauti tofauti za dunia, na ndio maana mara baada ya Trump kumaliza kile kiapo cha Urais cha maneno yale 35 pekee.. Na kumaliza kwa ile sentensi maarufu ya kwenye kiapo "…. so help me God!", Trump amekuwa ndiye binadamu mwenye nguvu zaidi kwa sasa juu ya huu uso wa dunia.

 
Kaangalie 24 series uone mambo ya Jack Bauer na hizo codes wanazo ongelea japo ni fiction ila dah hapana aisee sikumbuki ni season ipi ila kuna sehemu Air force one (The Angel) ilitunguliwa na gaidi mmoja Habib Maruan akafanikiwa kuipata ile black bag yenye hizo codes zikiwa kwenye mfumo wa kitabu kilochofuata hapo sikumbuki
 
Kama uliangalia vizuri kila rais wa Marekani anapotoka madaraka siku ya kuapishwa rais mpya hubaki peke yake ofisini na kuweka bahasha kwenye droo ya rais mpya. Unafikiri ile bahasha ina nini.
 
... Unafikiri ile bahasha ina nini.
Satanic verses I think. Kila taasisi ina top secrets zake; Imagine pale Vatican pana siri ngapi zimetunzwa pale for 2000 yrs now. Nenda pale Makka, inasemekana lile original jambia alilotumia jamaa liko pale linatunzwa balaa. Hata ndani ya familia ni hivyo hivyo; ili kusurvive siri ni lazima.
 
Hayo makombola 4500 yako tiyari? yaani ninkufyatuliwa tu? Halafu sio kwwli kwamba yanaweza teketeza Dunia na kumbuka nchi nyingi zina mifumo ya kujilibda pia.

Kuna Mahali nilisoma Pamoja na hizo Code lakini swala mfano la kushambulia nchi ambayo nayo ina nuclear ni gumu kidogo, kiasi kwamba zinahitajika idhini za bunge.

Kwa sababu kuna mambo ya kulipiza kisasi, maana yake na wao wategemee Mabomu ya Atomic kutua hapo New york
 
Na Urusi ana Dead Hand, ambayo ilikuwa enzi za USSR ingawa wachunguzi wanasema bado iko active, kwamba hata watu wote wakifa makombola yanaweza jifyatua yenyewe kwa kuhisi tu mtikisiko,
 
Hebu kuwa na aibu hata kidogo..

Huo mchezo unaoufanya wewe/mwenzako anayekuibia makala kutoka kwenye group la "Simulizi Za The Bold" alafi unakuja kuziweka huku bila aibu kujifanya za kwako siku zenu zinahesabika.. I'm tracking you down, soon mnakuwa removed from the group.. Ndani ya siku mbili tu nawatumbua..

Shame.!!
 
Kwahiyo now days story zako ni exclusive?......Kwamba huziweki tena in public bali ni kwa watu wachache?........Kwahiyo ndugu yetu huyu aliyetuletea mada ndio sababu ya wewe kufura povu?.........Hukutaka member wengine wasome hiyo habari?........Kama ulitaka, wangesomaje?
 
Nilikuwa najua ni makala yake.kumbe kakuibia.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…