Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Rais wa Marekani, Donald Trump, ameagiza ujenzi wa kituo cha kuwashikilia wahamiaji katika Kituo cha Guantanamo Bay, ambacho alisema kitakuwa na uwezo wa kuhifadhi hadi watu 30,000.
Alisema kituo hicho kilicho katika kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani nchini Cuba, ambacho kitakuwa tofauti na gereza lake la kijeshi lenye ulinzi mkali, kitawahifadhi "wahamiaji haramu wahalifu hatari zaidi wanaotishia watu wa Marekani."
Guantanamo Bay kwa muda mrefu imekuwa ikitumiwa kuhifadhi wahamiaji, jambo ambalo limekosolewa na baadhi ya mashirika ya haki za binadamu.
Baadaye Jumatano, "tsar wa mpaka" wa Trump, Tom Homan, alisema kituo kilichopo kwa sasa kitapanuliwa na kitaendeshwa na Idara ya Uhamiaji na Forodha (ICE).
ANGALIZO:
Trump hacheki na nyani; Watanzania mlioko huko chukueni hatua, msijepelekwa Guantanamo bay