Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Kwanini tupewe misaada kwanza?

Hivi kwanini pesa za kufanya mambo ya kipuuzi zinapatikana lakini pesa za kuhudumia raia tunategemea tusaidiwe na mataifa mengine?
 
Mkuu mataifa ya China na Russia watalitumia vizuri hilo gape, trump ni mwenda wazimu sana, Wenzake walikuwa wanazipembejea nchi duniani kwa mahusiano yeye ndio anaenda kuvunja, Trump sio mtu sahihi sana kwa uongozi wa Marekani
 
Warusi na wachina hawana pesa za kuchezea eti wakugawie ili uende kufanya mambo ya kipuuzi.
Hap watu wakikupa pesa usipo ilipa basi utaitapika kupitia matundu yote.
 
Kwanini tupewe misaada kwanza?

Hivi kwanini pesa za kufanya mambo ya kipuuzi zinapatikana lakini pesa za kuhudumia raia tunategemea tusaidiwe na mataifa mengine?
Swali zuri😍🤩
 
Warusi na wachina hawana pesa za kuchezea eti wakugawie ili uende kufanya mambo ya kipuuzi.
Hap watu wakikupa pesa usipo ilipa basi utaitapika kupitia matundu yote.
Nani kakwambia, inaonekana hufahamu sasaivi China na Russia mpango wao mkubwa ni kuzitoa nchi washirika wa Marekani ziwaunge mkono wao halafu waje wafanikishe kuanzisha hela yao ili iipiku marekani kiuchumi, Trump hapa ndio anaenda kuharibu mipango ya US iliyojengwa muda mrefu sana
 
Wazungu wanatumia hii misaada kwa makusudi tu ili kutulemaza tusiweze kujitegemea na kila siku tuwategemee.

Trump anayeifuta ndio anatutakia mema kwa sababu kwa njia hii anataka tujitegemee kwani hata wenyewe hakuna aliyewasaidia sasa kwa nini sisi tuwe watu wa kuendekeza tu misaada..!!??

Mbona nchi kama China na hata zile za kiarabu zenye utajiri mkubwa wa mafuta hazitoi hiyo misaada. Hakuna nchi duniani ambayo watu wake waliwahi kuwa na maisha bora kwa kusaidiwa. Hakuna.
 
Hayo mataifa unayoyasema hayana sera za kimarekani hata kidogo.. Unawajua China unawasikia.? We hushangai kwanini WHO wanatoa mchango mdogo vile.?

Huwezi kuitenga US hata kidogo Mkuu kwenye hii dunia ukata ujua hilo.


Angalia Ndani ya nchi yako kma Kuna barabara au mradi wowote ule wa kimaendeleo ya kudumu umefanywa nje na KWA MSAADA WA WATU WA MAREKANI.
 
Kwa hiyo misaada inayotolewa na USAID, mfuko wa PEPFAR ndio basi tena!? Miradi ya afya itaathirika, kuna ile ya kupambana na malaria, kifua kikuu, ukoma na UKIMWI siju kama serikali yetu ina uwezo wa kustahimili yenyewe bila misaada. Mazoea ya kusaidiwa ni mabaya mno, siku mwenye kutoa msaada akigoma huleta kizaazaa
 
Wewe acha kudanganya watu wanaokuzidi akili badala yake danganya wajinga.

China na Russia lini uliwahi kuona wanasaidia mataifa fukara. China aliwahi kutujengea reli na Zambia mwaka 1970 huko na ndio ikawa mwanzo na mwisho. Walikuwa na kiwanda cha nguo hapa Ubungo kikiitwa Urafiki wakakiua makusudi ili walete nguo kutoka China.

Russia ndio nyambole kabisa hata kiwanda kimoja hana ktk bara zima la Afrika na hata huko kwao na wenyewe wako hoi baada ya wawekezaji wote kukimbia.
 
Mkuu mataifa ya China na Russia watalitumia vizuri hilo gape, trump ni mwenda wazimu sana, Wenzake walikuwa wanazipembejea nchi duniani kwa mahusiano yeye ndio anaenda kuvunja, Trump sio mtu sahihi sana kwa uongozi wa Marekani

Havunji mahusiano na mataifa mengine, bali anachokifanya ni kukata misaada.

Kwani ndugu yako au jamaa zako wakisitisha misaada utawatenga au kuvunja mahusiano?
 
Umemaliza Kuota?
 
Nawaikate tuu
Sababu tunaishi kama omba omba miaka 64 ya uhuru hatuna hata kiwanda cha toothpick, tumebarikiwa madini, ardhi, mifugo, wanyama, misitu ila watu wanakula bata tuu mTanzania wa chini haneemeki na haya yote
Its time to wake up now... Lets vote wise otherwise tutakopa madeni yatakuwa makubwa wachina watakuja kututawala tena tuwe watumwa kwenye nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…