Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Katika mahojiano aliyofanyiwa rais mpya wa Marekani,Donald Trump hapo jana,amesema Marekani ina tamaa ya kuipata Green Land kwani wakazi wake takriban 50000 wote wanataka kuwa wamarekani.
Donald Trump hata hivyo hakufafanua umuhimu na haja ya kuwahamisha watu wa Gaza kwenda Jordan na Misri.
Trump says he believes US will 'get Greenland'
Akizidi kujibu maswali ya waandishi wa habari akiwa kwenye ndege ya uraisi ya Air force one,Trump amesema anakusudia kuisafisha Gaza yote na kwamba atawaomba raisi wa Misri Elsisi na mfalme wa Jordan,Abullah wawachukue watu wa Gaza kwa wingi kadri inavyowezekana.Donald Trump hata hivyo hakufafanua umuhimu na haja ya kuwahamisha watu wa Gaza kwenda Jordan na Misri.