Trump ayafanyia kampeni ya masoko magari ya Tesla ya Elon baada ya anguko kubwa la mauzo na hisa

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Baada ya anguko kubwa la mauzo na hisa za magari ya kampuni ya Tesla inayomilikiwa kwa hisa nyingi na kuongozwa Elon Musk, Rais wa Marekani Trump ameingia mzigoni akitumia ofisi ya Ikulu ya US, White House kuifanya matangazo ya kibiashara na kushawishi watu kununua magari ya Tesla huku akiwalaumu Democrats kwa kadhia ya kuanguka mauzo, hisa pamoja na uharibifu wa magari na miondombinu ya kampuni hiyo kote Marekani na Ulaya.

 
Nimeipenda hii;"In any event,I'm going to buy a brand new Tesla."

Magari ya Tesla ni rafiki wa mazingira,hayachafui mazingira.
 
Bangi zimempoza Musk, kwa matamushi na maamuzi yake ya kisiasa hakujua kama vitamgharimu?
 

Attachments

  • 7178e4c7-b41c-4cde-a0e1-0ad1469a1117.jpeg
    99.6 KB · Views: 1
Nimeipenda hii;"In any event,I'm going to buy a brand new Tesla."

Magari ya Tesla ni rafiki wa mazingira,hayachafui mazingira.
Hujaelewa sela za Trump? Kaiondoa Marekani kwenye mkataba wa Paris kuhusu mazingira, kasaini order ya kuruhusu ongezeko la uvunaji wa mbao akidai itasaidia kupunguza majanga ya moto😂😂😂
 
Walitaka kujikuta wao ndio wao sahivi sasa watakuwa wapole!.
na li X limehakiwa huko..🤣
oya hii dunia sahivi tunajionea matajiri na viongozi machachari kweli marekani imekuwa kama uwanja wa komedi!.

Sometimes the world is like a movie!, so other than chase it better stay and watch!
 
Sababu za kushuka kwa hisa za Tesla ni mchanganyiko wa mambo mbalimbali, ikiwemo:


Ushindani mkubwa kutoka kwa washindani wake kwa Makampuni mengine ya magari ya umeme, kama vile Rivian na Lucid Motors, yanazidi kushindana na Tesla na kuongeza shinikizo kwa kampuni hiyo.

Masuala ya utendaji wa kifedha Ingawa Tesla inajulikana kwa kuwa na faida nzuri, baadhi ya ripoti za kifedha zimeonyesha wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kubaki na ukuaji wa haraka, hasa katika masoko mapya.

Upungufu wa usambazaji na uzalishaji wenye changamoto za mnyororo wa ugavi (supply chain) zimeathiri uzalishaji na utoaji wa magari, hali inayosababisha kuchelewa kwa utoaji na kushuka kwa mauzo.

Matumizi ya fedha ya Elon Musk amewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika kampuni nyingine, kama SpaceX na Twitter (X), hali ambayo inaweza kuathiri mtaji na dhamira yake kwa Tesla.

Mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma za Tesla ilipandisha bei za magari yake, na baadhi ya wateja walijibu kwa kutoonyesha hamu kubwa ya kununua, jambo ambalo linaweza kuwa limeathiri mauzo.
 
Elon ndio Rais kivuli wa USA
 
Hii ni aibu na haimithiliki. Je, Rais anaweza kujidhalilisha kwa kujaribu kuokoa kampuni ya Elon Musk kwa kununua Tesla moja kwa moja ndani ya White House? Yeye kanunuq moja na mjukuu wake kamnunulia moja, huku Wamarekani wengi wakishangaa jinsi ya kuletea familia zao chakula kutokana na kupunguzwa kwa kazi kwa sababu ya Musk na Trump?

Kutumia uwanja wa White House kama eneo la kutangazia gari la kisasa kwa mtengenezaji wa magari ni matumizi mabaya makubwa ya rasilimali za umma, kana kwamba ni mali yake ya kibinafsi
 
Marekani imeharibika na inazidi kuharibiwa sana na Trump katika utawala wa sheria na siasa za kistaarabu.
 
Mungu aende na Rais Trump kwa kishindo kikuu. Mungu ambariki sana Rais Trump
 
Hiyo picha ya mwisho Trump hakujipanga kupiga picha aisee!
 
Mbona kitambo tunamjua ni mtumiaji wa jani, US sheria zinaruhusu. Huwa ni reference kwa watumia jani
Kutumia jani na kufanya maamuz ya kidwanzi ni vitu viwili tofauti..
ok anakula jani sio sababu ya kuwa mjingamjinga hata kama ana hela!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…