kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,846
- 20,319
Trump: Marekani ilimlazimisha Putin kuishambulia Ukraine
Rais wa zamani wa Marekani amesema kuwa, serikali ya sasa ya nchi yake ni mkosa na ndiyo iliyochochea mashambulizi ya Russia dhidi ya Ukraine.
Donald Trump amekuwa mmoja wa wakosoaji wakubwa wa Rais Joe Biden wa Marekani. Aidha Trump na Biden kuna uwezekano wakachuana tena katika uchaguzi wa Rais wa Marekani mwaka 2024.
Akizungumza katika mahojiano na televisheni ya Real America's Voice, Trump ameeleza kuwa: chombo kimoja cha habari cha mrengo wa kulia na chenye mfungamano na chama cha Republican kimeeleza kuwa, matamshi yaliyotolewa kabla ya kuanza vita huko Ukraine yalimpelekea Rais Putin achukue uamuzi wa kuishambulia kijeshi Ukraine.
Rais huyo wa zamani wa Marekani ameongeza kuwa: iwapo kadhia hii itachunguzwa tutaona kuwa ni wazi kwamba upande wa pili ndio uliomchochea Putin. Nchi au viongozi wangu ndio waliomchochea Putin kuishambulia Ukraine. Walimlazimisha kufanya hivyo; walitoa matamshi ya kipumbavu, amesema Donald Trump.
Katika mahojiano hayo, Donald Trump kwa mara nyingine amerudia kauli yake aliyoitoa katika miezi kadhaa iliyopita kwamba shambulio dhidi ya Ukraine lisingetokea kama angekuwa Rais wa Marekani.
Trump hakufafanua jinsi serikali ya Biden ilivyoilazimisha Russia kuishambulia Ukraine hata hivyo miezi kadhaa kabla ya kuanza vita huko Ukraine, serikali za Magharibi zilizungumzia suala la kujiunga Ukraine na Nato sambamba na kuendesha propaganda katika uwanja huo.