Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Ni kama Scenario ya Mgahawa..., kuna wateja wamekuja kuburudika sisi kama dunia (wenye mgahawa) kwa busara zetu tunajua wateja wote ni wafalme.., sasa kuna huyu mteja mmoja analeta sintofahamu ambapo kwa kauli zake ambazo zinafanya wengine wakereke, na washindwe kuendelea na mambo yao kama awali. Ukweli ni kwamba mgahawa sasa hivi upo katika sintofahamu
Urusi ni kama mteja fulani ambaye watu walishamuona kwamba ni mkorofi (iwe kweli au uongo) ingawa na yeye anaendelea kula nyama kimya kimya ila kuna wengine wanapenda sana kumsema vibaya na wanasema anakomba nyama za majirani zake lakini yeye hapigi sana kelele (na hapo nyuma kumbuka) hata USA ni mkomba mboga ila yeye alijua kula na vipofu kwahio wengi hawakulitambua hilo (yaani alikuwa mjanja mjanja)
Mchina ni kama mteja ambaye yeye haongei anakula zake nyama polepole tena nyingine za kutoka jikoni kabisa; wakati wengine wanapiga kelele na wengine wanalalamika kimya kimya kuhusu mpiga kelele yeye anatumia muda huo kula nyama
Ulaya ni kama wale wateja ambao ingawa wanakereka na mara nyingine kutemewa mate na mpayukaji ambaye akiongea hata kuna vimate mate anavitema wapo kimya tu wanashangaa...
Huku Mataifa mengine yaliyobaki wao wanalalamika kwanini huyu anaongea sana badala ya kula sababu kwa kula kwake kuna makombo yangeanguka na wao wangekula...., watu hawa hawajui kwamba kumbe nyama ya zile ng'ombe nyingine zinatoka kwao hivyo wangekuwa na busara wangechinja huyo ng'ombe kabla ya kumsafirisha....
Kwa maono yangu mteja anayenufaika hapa ni yule mchina anayeendelea kula wakati wengine wanashangaa shangaa, vilevile USA pia hafaidiki sababu hapo nyuma marais wengine walijua kula na vipofu (kimya kimya) huku wakitupa vimakombo huku na kule..., huyu anawagusa mkono vipofu hivyo kuwashitua na huenda kula yake ikapungua...