Trust na Vanessa Mdee wazindua rasmi Tamasha la "Divas Only" Dodoma, Mwanza na Mbeya

Trust na Vanessa Mdee wazindua rasmi Tamasha la "Divas Only" Dodoma, Mwanza na Mbeya

News TZ

Senior Member
Joined
Jun 17, 2015
Posts
132
Reaction score
75
attachment.php

Msanii Vanessa Mdee (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi mbalimbali wa Shirika la DKT International kabla ya kufungua rasmi Tamasha la Divas Only ambalo lilifanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Katikati) ni Meneja Masoko DKT International Sialouise Shayo.

attachment.php
Mshauri katika shirika lisilokua la kiserikali DKT International Mama Annet Mtuta akitoa ushauri kwa kina dada waliofika kuhudhuria uzinduzi wa tamasha la Divas Only ili kutoa elimu ya uzazi wa mpango lililofanyika jana jijini Dodoma.

attachment.php

Vanesa Mdee akitumbuiza katika tamasha la kutoa elimu ya uzazi wa mpango lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Tamasha lililopewa jina la ?Divas Only Concert? lilifanyika katika ukumbi wa Royal Village na kuratibiwa na Shirika lisilokua la kiserikali DKT International.

Mwishoni mwa wiki liliyopita TRUST walizindua mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya Divas Only ambayo yalimshirikisha mwanadada na msanii wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee. Trust ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa na wanawake kwa ajili ya wanawake.

Trust ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye. Madiva wa Trust wanafanya maamuzi na kupanga mafanikio yao ; Trust iko hapa kukusaidia katika safari hii. Tulifurahia shangwe tuliyopata na Vanesaa pamoja na Madiva wa Trust wa Dodoma. Kama wewe ni Diva wa Trust ama unataka kujua zaidi kuhusu , njoo ukutane na Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika matamasha yetu mengine Mbeya Desemba 04 pale Sunset Hall, Soweto na Mwanza Desemba 13, Malaika Beach Resort.

Huwezi kufika? Tafuta eneo lilipo Dodoma, Mbeya na Mwanza katika tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!
 

Attachments

  • 2.JPG
    2.JPG
    749.7 KB · Views: 472
  • 5.jpg
    5.jpg
    392.3 KB · Views: 385
  • 6B.jpg
    6B.jpg
    377.7 KB · Views: 391
Back
Top Bottom