Try again: Manzoki alisaini Simba

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Mwenyekiti wa bodi ya Simba Salim Abdallah Try Again amesema Cesar Lobi Manzoki alisaini mkataba wa awali Simba (Pre contract) lakini baada ya kusaini mkataba na klabu ya hiyo, Manzoki alipata ofa nzuri zaidi ambayo analipwa mara sita zaidi ya wao walivyotaka kumlipa hivyo mchezaji aliomba aende China, na wao kama binadamu waliona ni bora wamruhusu kwasababu wachezaji wanategemea mpira kuendesha maisha yao hivyo basi sio vema kumzuia mchezaji kwenda sehemu ambayo atapata maslai zaidi.

“Manzoki alishasajili mkataba wa awali (pre-contract Simba) lakini yule ni binadamu, ni mchezaji ana career yake. Akatuomba, nimepata ofa China, nalipwa mshahara mara sita ambao mtanipa nyinyi. Mshahara wake kule ni Euro 60,000. (TSH150M kwa mwezi) Kama ubinadamu unafanyaje na yule ni mchezaji? Wewe hauna uwezo wa kumlipa Euro 60,000, unamruhusu!” alisema Salim Abdallah 'Try Again'
 
Sijui anatukadiliaje[emoji23][emoji23]
Mwanzo walitudanganya

Pili,wakamleta kama special appearance kwenye uchaguzi(kuhadaa)

Tatu, kauli hii Tena Leo kuelekea dirisha la usajili Tena KUBWA

NB ,Simba Tunatakiwa kuwa makini mno na Hawa watu


Mtu mwenyewe jina la utani TRY AGAIN nasimba imeshajaribu Sana Sana Sana imetosha
 
Kabisa mkuu.... management inafeli
 
Mbumbumbu anakuaje na akili?
 
Waache maneno mengi waondoe mizigo walete vyombo.

Tunaaibika sisi
 
Sawa Manzoki alipata timu inamlipa zaidi na Try Again na Simba yake wakamwachia aende kwenye maslahi zaidi; swali la msingi badala yake walimsajili nani kuja kuchukua nafasi yake? Au ndio Dejan?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…