Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 87
Whaaaaaat? Sasa JK hayuko serious...wadau hebu mwenye CV ya huyu mkuu atupe.Ambassador?
huyu jamaa ni failure mtupu, ilala wananchi walimkataa huyu, km sikosei ilikuwa sakata fulani la ardhi
Whaaaaaat? Sasa JK hayuko serious...wadau hebu mwenye CV ya huyu mkuu atupe.Ambassador?
Kumbe hiyo CV yake hata wewe huna, sasa kinachokupayusha 'whaaaaaat' ni kitu gani?
By the way kwenye ubalozi kuna kitu gani cha tija sana? bora kuwa wachapakazi watakaokuwa wilayani kusukuma maendeleo ya wananchi mbele na waliochoka wapelekwe kwenye balozi chovuchovu kama burundi, malawi, zimbwi n.k. Kwangu mimi naiona nafasi ya ukuu wa wilaya kuwa ya manufaa zaidi kwa Watanzania kama tutapata mchapakazi kuliko kuwa na mchapakazi balozi nchini malawi.Shida nyingine ni kuwa wakuu wa wilaya wapo kwa matwaka ya kisiasa na wala sio kwa ajili ya maendeleo ya watanzania husikaMimi ninavyomjua huyu mkuu alikua mkuu wa wilaya,sasa kweli ni ishu gani iliyomsukuma jk aone anaweza kuwa ambassador uko malawi?Hebu tunaomba CV yake kitaaluma coz ukuu wa wilaya tu ndo umemfanya awe qualified kuwa balozi?Huoni tatizo hapo?
Kwa anayesema malawi hatuna serious issue nayo9 simwelewi pia,unajua nchi kama malawi iko ktk strategic location?
Tuna watanzania wanafanya biashara malawi,and there are still some more opportunities kwa watanzania kuwekeza kule
Pia Tunahitaji wateja kwa ajili ya bandari zetu ingwa ziko hoi,pia cooperation in defence nk....usiseme hatuna ishu serious na malawi,basi ubalozi wetu huko ufungwe?
Hayo ndiyo maajabu ya JF siku hiziKumbe hiyo CV yake hata wewe huna, sasa kinachokupayusha 'whaaaaaat' ni kitu gani?
By the way kwenye ubalozi kuna kitu gani cha tija sana? bora kuwa wachapakazi watakaokuwa wilayani kusukuma maendeleo ya wananchi mbele na waliochoka wapelekwe kwenye balozi chovuchovu kama burundi, malawi, zimbwi n.k. Kwangu mimi naiona nafasi ya ukuu wa wilaya kuwa ya manufaa zaidi kwa Watanzania kama tutapata mchapakazi kuliko kuwa na mchapakazi balozi nchini malawi.Shida nyingine ni kuwa wakuu wa wilaya wapo kwa matwaka ya kisiasa na wala sio kwa ajili ya maendeleo ya watanzania husika
Mi nadhani Balozi wetu huko Malawi lazima aelewe kuwa kumekuwa na dispute ya muda mrefu kuhusu ulipo mpaka wetu Ziwa Nyasa (wao wanaita Malawi)...wakati sisi tunajua unapita kati kwa kati, wao wameona ziwa lote upande wa Tanzania ni la kwao.
je huyu ataweza kusukuma suala hilo pamoja na mengine yakiwamo ya detention za gafla gafla za wafanyabiashara wa TZ huko Malawi?
Mkuu,
Hasa katika defence cooperation,yaani kuwa mkuu wa wilaya ambaye kiitifaki ndiye mwenyekiti wa kamati za ulinzi za wilaya ndiye anapelekwa kuwa head of our mission abroad?
Ndo maana nikahitaji hata CV yake ili tuone ana nini huyu mkulu otherwise Jk atakua incompetent in appointing our foreign envoys!
Kwanza amekua foreign ministers for ten years bila shaka anajua foreign policy yetu kwa malawi ni nini,na pia foreign policy ya malawi kwetu ni nini.
Pia i hope amezingatia maslahi yetu huko SADC na maslahi ya watanzania kiujumla huko Malawi.So,kama alifikiria haya yote ndipo alipomteua mkuu wa wilaya Patrick Tsere akaona uwakilishi wake ktk wilaya ya ilala ni sawa na kuongoza foreign mission yetu nje!
Wana JF mliochangia Patrick Tsere ninayemjua mimi si huyo ambaye baadhi yenu mmekuwa mkimuelezea with an exception of De Novo. Tsere ambaye Baba yake mzazi alikuwa miongoni mwa madaktari wa awali hata kabla Tanzania haijapata uhuru, alipata formal education kuanzia primary, middle school, secondary (O level) na High School (A level). Baadaye akaenda IDM Mzumbe alikopata Diploma in Public Administration na baadaye akapata Post Graduate Diploma in Management. Aidha anayo MA in Diplomacy.
Amefanya kazi kama Afisa Mipango Wilaya ya Iringa; Manpower Officer Wizara ya Mipango na Uchumi; Wizara ya Mambo ya nchi za Nje (mwaka 1983 hadi 1996 kama Afisa wa Ubalozi ubalozini nchini Zambia wakati huo Ubalozi wa Tanzania ulikuwa pia unatuwakilisha nchi ya Malawi na Botswana); Akaja kuwa in charge of operations idara ya Wakimbizi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 1997 to 2002; 2002 to 2005 akawa CEO wa AICC Arusha baadaye akaenda kugombea ubunge kwao Karatu. 2006 hadi 2009 akawa DC Ilala.
Kwa ufupi hiyo ndiyo CV ya Tsere. Sasa kama inakidhi hizo concerns zenu ninaamini ndani ya CV hii mtapata majibu. Kwa mfano tatizo la mpaka kati ya Malawi na Tanzania hilo ni tatizo tangu enzi za Mwalimu. Sitaki kuamini kuwa Tsere halijui kwa vile akiwa afisa ubalozini Lusaka, nchi ya Malawi ilikuwa sehemu ya brief ya ubalozi wetu na sina shaka tatizo hilo atakuwa analifahamu vizuri sana.
Bila shaka CV hii itakupeni picha ya kuwa Tsere hakubebwa. Ni dhahiri he is fit for the job as he has the required qualifications as well as the expertise, na aliempa hiyo kazi hakukosea. Ninawaomba wanaJF wenzangu kumbukeni ule usemi "No research no right to speak"