Tsh. Bilioni 290 kuimarisha Usimamizi wa Taka Ngumu katika Halmashauri za Dar

Tsh. Bilioni 290 kuimarisha Usimamizi wa Taka Ngumu katika Halmashauri za Dar

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini TARURA kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam Awamu ya Pili (DMDP Phase II), umepanga kutumia Tsh. bilioni 290 katika uimarishaji na usimamizi wa taka ngumu katika Halmashauri tano za Mkoa wa Dar es salaam.

Mratibu wa Mradi wa Benki ya Dunia, Mhandisi Humphrey Kanyenye amesema hayo alipokuwa akitoa taarifa fupi ya utekelezaji wa DMDP awamu ya pili katika hafla ya utiaji saini wa mikataba ya awali ya ujenzi wa barabara katika Halmashauri tano za Mkoa wa Dar es salaam, katika viwanja vya Mwembeyanga, Manispaa ya Temeke.

“Gharama za utekelezaji wa mradi wa DMDP awamu ya pili ni trilioni 1.182, asilimia 25% ya fedha za mradi sawa na Tsh. bilioni 290 zitatumika katika usimamizi wa eneo la taka ngumu tofauti na awamu ya kwanza ambapo halikufanyiwa kazi katika suala la ukusanyaji, usafirishaji na kuzihifadhi taka ngumu katika madampo ya kisasa’’

Mhandisi Kanyenye amesema mradi umewekeza nguvu katika usimamizi wa taka ngumu katika awamu ya pili ili kuboresha eneo hilo katika Mkoa wa Dar es salaam kwa kuwekeza kwenye miundombinu ya ukusanyaji, usafirishaji pamoja na kuhifadhi taka ngumu katika madampo ya kisasa tofauti na awamu ya kwanza ambapo mradi ulijikita katika ununuzi wa magari na ujenzi wa vizimba na mradi utaboresha programu mbalimbali za usimamizi wa taka ngumu ikiwemo kandarasi za ukusanyaji wa taka ngumu na kuchochea urejeshaji wa taka ngumu (Recycling), na utasaidia kuanzishwa kwa Taasisi ya mashirikiano ya Halmashauri zote tano za Mkoa wa Dar es salaam ambayo itasimamia taka ngumu tofauti na sasa ambapo kila Halmashauri ina utaratibu wake wa usimamizi jambo linalopelekea kukosekana kwa ufanisi wa usimamizi wa taka ngumu.

“Katika mradi huu wa uendelezaji Jiji la Dar es salaam awamu ya pili, madampo matatu ya kisasa yatajengwa ili kukabiliana na usimamizi wa taka ngumu katika Halmashauri zote tano katika Mkoa wa Dar es salaam na hivyo kuongeza ajira pamoja na ukuzaji wa uchumi kwa Wananchi wa Mkoa Dar es salaam”
 
Back
Top Bottom