Tsh Milioni 20 Niwekeze wapi kati ya bar/lounge au barbershop

Samahani mkuu, utanivumilia.

Wekeza kwenye kilichozalisha hiyo milioni 20.

Kama ni mkopo uliokopa ili ufanye biashara, hiyo biashara imeshakufa before it starts. Kwasababu umekopa ukiwa hujui ufanye biashara gani, na huwa tunakopa kuendeleza, sio kuanzisha. Sasa kwa swali lako, hata plan huna.

Kama ni savings, rejea lengo lako la kusave. Usichanganyikiwe ukadhani ni nyingi kiasi cha kuanza kuomba ushauri kwa umma. Kama ulisave bila mpango endelea tu kuzitunza, matatizo yapo, yanakuja kuzisomba.

Kama ni dili ulipiga, au kama ni kwa namna yoyote ile hiyo pesa ikawa ya mkupuo usio na jasho jingi au mipango ya baadae; toa zaka kwa imani yako, toa kiasi flani cha shukrani kwa imani yako, kiende kwenye madhabahu ya imani yako, iwe ni mganga wako, ama ule mbuyu mkubwa pale njia ya kwenda kwenu, au ni ile njia panda tunayokutaga nazi na mayai, au kanisani au msikitini. Muombe muweza wa imani yako aikumbuke sadaka yako. Kama ni atheist, huna imani yoyote, hakikisha kiasi hicho kinafikia wenye uhitaji, hapa kuna yatima, familia duni, huko vituoni, ila kiasi hiki usiwape walio wako, ndugu, binamu, dada yako mwenye hali duni, kwasababu kama wanakujua watakusifia na hawatakiwi, wewe sio wakusifiwa. Kama una moyo wa kusaidia walio wako, toa kiasi kingine tofauti na hiki.

Usishituke, si hela imekukuta hauna mpango, Kiasi flani kiende kwa wazazi (kama wapo), au walezi ambao ni chimbuko lako, ukiweza usitume kwenye simu au benki, peleka kwa mikono yako (ofcoz kwa mil 20 unafika popote tanzania bila kuitikisa sana, ikiwa tu, ni chimbuko lako) Usidharau nguvu ya kwenda physically, ila ni kama una nafasi.

Ukimaliza haya, hela yako itakua kwenye ulinzi dhidi ya miluzi. Najua unawaza barbershop au bar ila kuna ile miluzi ya "biashara ya hardware inalipa sana," "ukilima kitunguu saumu misimu miwili tu we sio mwenzetu," "weekend ijayo element kuna bendi kali," ama ile miluzi ya bebi wako ambayo we mwenyewe unaijua. Amini usiamini, hii miluzi bila ulinzi ina matokeo.

Nilisema univumilie kwasababu mimi sitachangia kwenye bar ama barbershop wala kukupa wazo la biashara. Ila mchango wangu ni kuhakikisha chochote unachofanya, hela yako inakua salama.

Usiidharau nguvu ya kutoa. Hayo yote niliyosema hapo ni matoleo.

Ukitekeleza hayo kwa moyo, amini nakuambia, kudra za muweza wako + shukrani za uliowapa kwa moyo. Kutoka ndani yako(nafsini mwako), litakuja jambo moja thabiti la kufanya, hutajisikia kusita, wala kuhitaji mawazo mbadala. Sio lazima liwe kati ya bar au barbershop, linaweza lisiwe wazo la biashara kabisa.

Ngoja niishie hapa, uniwie radhi kama ujumbe haujakufaa.
 
Nimekukuwa nikitamani sana kuwekeza kati ya hizi biashara mbili, wenye uzoefu na hizi biashara mnanishauri nini? Mambo gani ya msingi nizingatie kabla ya kuanza?

NB; Kutokana na ubusy nilionao sitaweza kuwa na usimamizi wa karibu. Nipo Dsm

Nakaribisha maoni yenu.
Nakuamisha kutoka dar es salaam nakuleta mbeya vijijini , uko tayari kaka ?
Huku bar zipo ila sio bar zile bar tunazozijua huko dasalam , sasa iko hivi njoo ukodi sehemu ufungue kibar fulani cha classic sababu huku hazipo , biashara ni uhakika sababu ya walevi kuwa wengi na ushamba wa wadada wazuri nakuhakikishia kupata hela

Zingatia kuwa huku kunakuwa na minada ambayo ipo maeneo tofauti hivyo fungua sehemu ambayo mnada wake ni mkubwa ambao hufanyika kila jumanne

Ili biashara yako yako ya bar iwabambe sana

1/ zingatia kuleta wadada wazuri hata watatu ila wasijue kulinga kwa mteja .

2/Hakikisha una vinywaji ambavyo vinapendelewa .

3/weka sehemu ya hadhi na changanyikeni .

4/uwe na msimamizi madhubuti anayewajua vyema watu wa pande hizo .

5/Usafi wa mandhari na lugha nzuri kwa wateja kutakulipa within a year hiyo hela yako .

Huku si wakulima wala wafanyakazi wote bar ni sehemu ya maisha , kinachokosekana ni huduma bora na sehemu mahususi ya kufurahia vilivyo bila kusahau huku kuna uchimbaji wa marumaru.

Karibu sana .
 
Hizi mada za kukamata mamilioni zimeshika kasi sana hapa jamvini awamu hii ya sita.
Hongereni miamba.

Kipindi cha JPM ilikuwa ni nadra sana kuona mada kama hizi.
 
Nakuamisha kutoka dar es salaam nakuleta mbeya vijijini , uko tayari kaka ?
Huku bar zipo ila sio bar zile bar tunazozijua huko dasalam , sasa iko hivi njoo ukodi sehemu ufungue kibar fulani cha classic sababu huku hazipo , biashara ni uhakika sababu ya walevi kuwa wengi na ushamba wa wadada wazuri nakuhakikishia kupata hela

Zingatia kuwa huku kunakuwa na minada ambayo ipo maeneo tofauti hivyo fungua sehemu ambayo mnada wake ni mkubwa ambao hufanyika kila jumanne

Ili biashara yako yako ya bar iwabambe sana

1/ zingatia kuleta wadada wazuri hata watatu ila wasijue kulinga kwa mteja .

2/Hakikisha una vinywaji ambavyo vinapendelewa .

3/weka sehemu ya hadhi na changanyikeni .

4/uwe na msimamizi madhubuti anayewajua vyema watu wa pande hizo .

5/Usafi wa mandhari na lugha nzuri kwa wateja kutakulipa within a year hiyo hela yako .

Huku si wakulima wala wafanyakazi wote bar ni sehemu ya maisha , kinachokosekana ni huduma bora na sehemu mahususi ya kufurahia vilivyo bila kusahau huku kuna uchimbaji wa marumaru.

Karibu sana .
Asante sana mkuu, Mbeya mimi ni mwenyeji kiasi chake, nitafanyia kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani mkuu, utanivumilia.

Wekeza kwenye kilichozalisha hiyo milioni 20.

Kama ni mkopo uliokopa ili ufanye biashara, hiyo biashara imeshakufa before it starts. Kwasababu umekopa ukiwa hujui ufanye biashara gani, na huwa tunakopa kuendeleza, sio kuanzisha. Sasa kwa swali lako, hata plan huna.

Kama ni savings, rejea lengo lako la kusave. Usichanganyikiwe ukadhani ni nyingi kiasi cha kuanza kuomba ushauri kwa umma. Kama ulisave bila mpango endelea tu kuzitunza, matatizo yapo, yanakuja kuzisomba.

Kama ni dili ulipiga, au kama ni kwa namna yoyote ile hiyo pesa ikawa ya mkupuo usio na jasho jingi au mipango ya baadae; toa zaka kwa imani yako, toa kiasi flani cha shukrani kwa imani yako, kiende kwenye madhabahu ya imani yako, iwe ni mganga wako, ama ule mbuyu mkubwa pale njia ya kwenda kwenu, au ni ile njia panda tunayokutaga nazi na mayai, au kanisani au msikitini. Muombe muweza wa imani yako aikumbuke sadaka yako. Kama ni atheist, huna imani yoyote, hakikisha kiasi hicho kinafikia wenye uhitaji, hapa kuna yatima, familia duni, huko vituoni, ila kiasi hiki usiwape walio wako, ndugu, binamu, dada yako mwenye hali duni, kwasababu kama wanakujua watakusifia na hawatakiwi. Kama una moyo wa kusaidia walio wako, toa kiasi kingine tofauti na hiki.

Usishituke, si hela imekukuta hauna mpango, Kiasi flani kiende kwa wazazi (kama wapo), au walezi ambao ni chimbuko lako, ukiweza usitume kwenye simu au benki, peleka kwa mikono yako (ofcoz kwa mil 20 unafika popote tanzania bila kuitikisa sana, ikiwa tu, ni chimbuko lako) Usidharau nguvu ya kwenda physically, ila ni kama una nafasi.

Ukimaliza haya, hela yako itakua kwenye ulinzi dhidi ya miluzi. Najua unawaza barbershop au bar ila kuna ile miluzi ya "biashara ya hardware inalipa sana," "ukilima kitunguu saumu misimu miwili tu we sio mwenzetu," "weekend ijayo element kuna bendi kali," ama ile miluzi ya bebi wako ambayo we mwenyewe unaijua. Amini usiamini, hii miluzi bila ulinzi ina matokeo.

Nilisema univumilie kwasababu mimi sitachangia kwenye bar ama barbershop wala kukupa wazo la biashara. Ila mchango wangu ni kuhakikisha chochote unachofanya, hela yako inakua salama.

Usiidharau nguvu ya kutoa. Hayo yote niliyosema hapo ni matoleo.

Ukitekeleza hayo kwa moyo, amini nakuambia, kudra za muweza wako + shukrani za uliowapa kwa moyo. Kutoka ndani yako(nafsini mwako), litakuja jambo moja thabiti la kufanya, hutajisikia kusita, wala kuhitaji mawazo mbadala. Sio lazima liwe kati ya bar au barbershop, linaweza lisiwe wazo la biashara kabisa.

Ngoja niishie hapa, uniwie radhi kama ujumbe haujakufaa.
Shukran mkuu kwa angalizo...

Bado nafanya hiyo shughuli, lengo ni kufanya diversification tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukimaliza haya, hela yako itakua kwenye ulinzi dhidi ya miluzi. Najua unawaza barbershop au bar ila kuna ile miluzi ya "biashara ya hardware inalipa sana," "ukilima kitunguu saumu misimu miwili tu we sio mwenzetu," "weekend ijayo element kuna bendi kali," ama ile miluzi ya bebi wako ambayo we mwenyewe unaijua. Amini usiamini, hii miluzi bila ulinzi ina matokeo.
We jamaa uko vizuri kichwani
 
Kwa uchumi huu hakuna mtu mwenye kutengeneza Milioni 20 halafu akose cha kufanyia. May be ni pesa ya wizi, urithi, ya kuokota au ya walamba asali.
 
Nimekukuwa nikitamani sana kuwekeza kati ya hizi biashara mbili, wenye uzoefu na hizi biashara mnanishauri nini? Mambo gani ya msingi nizingatie kabla ya kuanza?

NB; Kutokana na ubusy nilionao sitaweza kuwa na usimamizi wa karibu. Nipo Dsm

Nakaribisha maoni yenu.
Mimi nakuja na wazo jipya. Nimezingatia umesema huna muda mwingi wa kusimamia kwa ukaribu. Ni hivi: Anza biashara ya kutuma na kupokea fedha BILA TOZO. Anza kwa kufungua vibanda viwili vya kutuma na kupokea fedha i.e. M-pesa, Tigo nk. Tafuta wadada wawili waaminifu waweke. Kibanda cha kwanza kiweke Dar na cha pili kiweke mkoani eg Mwanza. Cha kuzingatia ni kuwa weka vibanda vyako kwenye mikoa miwili yenye mizunguko ya fedha kwa wingi. Ifanye biashara ya M-pesa nk kama cover-up tu na usiizingatie sana. Kazi yako kubwa iwe ni kutuma na kupokea fedha BILA TOZO, huku ukichukuwa ADA yako kidogo. Kibanda cha Dar weka sh milioni kumi. Cha mkoani weka sh milioni kumi. Fanya kazi kwa akili. Akija mteja kutuma fedha mkoani, msome, ukione anaingilika mwambie utamsaidia kutuma BILA TOZO, ila utachukuwa ada yako kidogo sana. Akikubali mwambie akupe jina la mpokeaji na fedha anazotaka kutuma. Ukilipata piga simu au msg ya Whatsup kwa mtu aliyeko kibanda cha mkoani, mwambie amlipe huyo mpokeaji. Mpango mzima ni kuwa fedha hazitumwi physically bali kwa maelekezo. Na wa mkoani naye akitaka kutuma inakuwa hivyo hivyo, huku wewe ukichukuwa fee yako.
 
Shukran mkuu, bonge la wazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom