Tsh milioni 60 shwaaa zikapotea!

Armani William

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2014
Posts
248
Reaction score
744
Starehe mnazipenda ila mwisho wake MBAYA. Wengi wameteketea kwa kuendekeza UMALAYA.

Ishi vizuri, kula vizuri, fanya mazoezi na umrudie Muumba wako.

___________________________________________________________

Nikiwa na miaka 24 pindi tu baada ya kuhitimu elimu yangu ya chuo kikuu niliingia mtaani, akilini na moyoni nikiwa na hari ya kuanzisha kampuni yangu. Ndoto niliyokuwa nayo tokea naingia form 3 ambapo niliacha masomo ya sayansi na kufwata kile moyo ulichoniambia KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA.

Basi bana mwaka wa kwanza ukaisha nipo kitaa, moja haisimami mbili haikaii. Mwaka uliofwata nikiwa mtaani, nikaaanda mpango wangu biashara (ambao kwa sasa nikiusoma naona makosa mengi sana) nikaongea na wadau wawili watatu kupata mtaji wa biashara. Mungu si athumani wala hadija nikafanikiw kupata mtaji wa shillings 60,000,000.

Nikaingia kwenye biashara ya ununuzi (ulanguaji al-maarufu KANG'OMBA) korosho huko Mtwara wilaya ya Masasi. Simu wa kwanza mambo yalienda vizuri hela ilirudi. Nikaamua kwenda Uganda kufanya utafiti biashara ya mchele kule sasa mambo ndipo yaliponiendea kidogo kombo maana nilianza kupoteza taratibu pesa.

Long story short, nilikuja kupoteza pesa Million 60 shwwaaaaaa zikapotea zoootee kwenye korosho pale mzee baba (sijui huko alipo ni kiongozi wa malaika au anapigwa kama ngoma) aliposema serikali inaubavu wa kununua korosho (nyooo walijuta kilichowakuta).

Nilikaa kitaa miaka 7 sina uelekeo zaidi ya kuwa chawa kwa mwanangu wa ukwelii. Ila nilichojifunza ukianguka chukua muda kunyanyuka angalia mazingira ulipodondokea ukiwa bado chini, yatathmini mazingira husika kisha ndio unyanyuke.

IMEKUWA MAUMIVU MAZITO ILA AKILI YA KUYASHINDA NILIJAALIWA NA MUNGU.
 
Sikia stori za kuanguka kimaisha hapa JamiiForums tu, lakini yakikukuta kweli hata wazee wako utawaona wachawi wako.😂
 

Story yako umetia chumvi japo lengo la kutia chumvi linajulikana

Nov. 2018 serikali ndio ilitangaza kununua korosho ( mpaka sasa miaka minne tu imepita) ila wewe umeshakaa miaka 7
 
Soma alichoandika mkuu,

Usibishebishe tu wengine hupenda kufupisha story sio waandishi wa story ndefu km alivyo DeepPond au IBRA wa PILI kua muelewa basi
Kufupisha Ni kukata baadhi yavitu ambavyo sio vya muhimu , mfano kwenye harakati za kununua korosho unakuta Kuna siku ulishabakwa hio unaweza iacha ukaendelea na point umepotezaje hio milion 60

Huwezi andika heading "namna nilibakwa" afu ndani ukaandika et kufupisha stori niliumia Sana 🤔
 
Ila magufuli alijua kuumiza watu kwenye korosho na bado hawakuziuza...
Mitaji ya watu wwngi sana ilienda na bado hawakulipwa.
Hawatamsahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…