mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 809
- 729
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imefanya mkutano na Mabalozi wa Tanzania wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi zilizopo kanda ya Asia na Australasia kwa lengo la kuimarisha mikakati thabiti ya utekelezaji wa kuvitangaza vivutio vya utalii wakati wa kipindi hiki ambapo sekta ya utalii duniani imeathirika na janga la Corona.
Mkutano huo uliyofanyika kwa njia ya mtandao uliendeshwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB, Jaji Thomas Mihayo na kuhudhuriwa na Mabalozi wa Tanzania wa ukanda huo; Mhe. Balozi Dkt. Ramadhani Dau wa Malaysia, Balozi Mbelwa Kairuki wa China, Balozi Baraka Luvanda wa India, Balozi Matilda Masuka wa Korea Kusini, Balozi Hussein Kattanga wa Japan, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia, Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Caesar Waitara pamoja na Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT), Dkt. Abdulla Juma.
Akifungua mkutano huo, Jaji Mihayo aliwasihi Mabalozi hao kutumia hadhi zao za kibalozi katika kuwahamasisha na kuwavutia watu mashuhuri, wanamuziki, wanasiasa na mabalozi wenzao wa nchi wanazofanyia kazi ili waje Tanzania kuvitembelea vivutio vya asili.
Katika mkutano huo ulioandaliwa na kuratibuwa na TTB, Mkurugenzi Meendeshaji wa TTB, Bi. Devota Mdachi aliwasilisha andiko (presentation) linaloonesha hali ya utalii wa Tanzania kwa sasa na mikakati iliyoanza kutekelezwa ya kutangaza utalii wa Tanzania katika kipindi hii ambacho nchi nyingi zimefunga mipaka yao.
Juhudi na mkikakati iliyojadiliwa katika mkutano huu unatarajiwa kuongeza idadi ya watalii kutoka katika masoko hayo. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii zinaonyesha mwaka 2018 Tanzania ilitembelewa na watalii 79,852 kutoka ukanda huo wa Asia na Australasia.
TTB inatarajia kufanya mkutano kama huo na mabalozi wa ukanda wa ulaya hivi karibuni ikawa ni muendelezo wa mikakati ya kujipanga vizuri katika kutangaza utalii wa Tanzania baada ya janga la Corona.