TTCL CEO awe Kevin Twisa

Kitu ambacho hatutakiwi kusahau ni kuwa makampuni yote binafsi yana culture zake ambazo mtu smart anaweza kuonyesha uwezo wake. Kuongoza haya mashirika ya umma, ambayo yamejaa mchanganyiko wa kila aina ya watu sio kitu rahisi. Makampuni haya kwa muda mrefu yalikuwa hayaongozwi na culture ya deliver in order to grow. Ni majungu na kujuana na ukubwa usio na kichwa wala miguu.
Jamani, sidhani kama Twisa amekomaa kiasi hicho katika kuongoza na kutoa maamuzi ambayo yataifanya TTCL iendelee kufanya kazi bila kuanguka.Tumpe muda akue kue kidogo, vinginevyo tutakuja kumpa lawama asizostahili
 
sio sahihi kabisa,´Huyo jamaa hawezi, kama alikuwa lulu mbona Tigo walimtimua? Mtu akishaonyesha makeke kwenye vyombo vya habari sio kigezo chakuweza kila kitu wandugu

Charles Keenja alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya jiji alifanya mambo mazuri saana na kila mtu akamsifia, waungwa wakamshauri kagombea ubunge, kutokana na hayahaya mnayoyasema hapa kapewa uwaziri wa kilimo mbona alichemsha?
 
ttcl?!!!

kufanya nini huko, hawana matangazo ya biashara ya maana kitu amabacho kelvin amebobea,
siasa nyingi kule nk nk nk nk
 
TTCL licha ya ukubwa wake, pia kuna ubwana na utwana mwingi.

Kuiongoza hiyo kampuni kwa ufanisi inahitaji mtu aliyesomea biashara, lakini mwenye holistic view. Marketing peke yake, au Engineering tu haitoshi.

Point ya mleta mada naiona. Kwani pamoja na TTCL kuja na vifurushi vingi vya intaneti, havitangazwi ipasavyo. Kwa mfano, wana package moja kwa ajili ya mashirika ya kiserikali na umma. Ina spidi nzuri (live video kama mchezo). Ni unlimited (1G), na bei yake kwa mwezi ni Tsh 1M. Binafsi nafahamu wizara kadhaa (tena zingine nyeti) na vyuo vya elimu ya juu vya umma vingi havitumii TTCL kama ISP. Wanao wahindi na huduma zao za kibabaishaji, kwa gharama ya zaidi ya Tsh 3M kwa mwezi. Nilishangaa na kusikitika. Naamini Twisa anaweza kufaa kama marketing manager.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…