TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Tatizo linaweza kuwa ni ubora wa simu wanazotumia, sijaitaja tecno Tafadhali sana.

Hahahaha mkuu una utani na watumiaji wa tecno! Na kweli simu pia zinachangia wenye simu zetu hizi ambazo hazisupport 4G network lazima iwe shida kidogo so mie naona kabla hatujalalamika tuangalie na aina za simu tunazotumia!
 
Kumbe inajiweka roaming ukisafiri sijawah kujua hilo
Duuh poleni! Sema mimi inachonikera ni kuweka ile data roaming ukiwa unasafiri japo maeneo kama Mbeya na Kyela nako inakamata vizuri tu!
 
Nyie TTCL mmechoka tu,siwe wakazi wa Ilemela pande hizi za karibu na ofisi za manispaa hakuna 3g mtandao unajikongoja kama Kobe mzee,line yenu ninayo ila hainipi mzuka wa kuitumia kwa jinsi internet yenu ilivyo mbovu
 
Kumbe inajiweka roaming ukisafiri sijawah kujua hilo

Yeah kwa hizi safari za mikoani mkiwa mnapita sehemu zenye mapori au milima huwa inaweka R pale juu ya kimnara chake hivyo mtandao unakuwa haukamati hadi uwashe data roaming ambayo inacost additional charges!

Ukifika sehemu unayoenda ndiyo inarudi kawaida!
 
Ooh okay hapo nimeelewa huwa inafanya hivyo sijawahi kuweka hiyo data roaming muda huo ikiwa haishiki naangalia tv ya bus .
 
Ooh okay hapo nimeelewa huwa inafanya hivyo sijawahi kuweka hiyo data roaming muda huo ikiwa haishiki naangalia tv ya bus .

Yes hata mie kwa muda ambao ninasafiri huwa siwashi naacha hivyo hivyo maana haina umuhimu na pia unaweza ukawasha na bado network ikasumbua vile vile!

Ila mie kile ki R tu kukaa pale juu ndiyo huwa kinanikera basi tu sijui huwa naonaje yaani halafu kingine TTCL ukiiweka kwenye baadhi ya viswaswadu (visimu vidogo) haiandiki TTCL inaaandika TIGO - TZ kwahiyo hili nalo itabidi watupe ufafanuzi aise!
 
Hii laini inachosha basi tu safari nzima network inazingua . Kumbe inaandikaga hivyo aisee .
 
Yeah huwa inaandika hivyo! Yaani hawa kuna muda wanazingua sana hivyo kuna wakati nawaelewa hawa wateja wanaowalalamikia!
Post za malalamiko ni nyingi kuliko maelezo ... Kuna siku nilikuwa natuma sms ndefu kwa mtu kumuelezea Jambo fulani nashangaa sms haiendi kumbe kuna limit ya 150 characters aisee
 
hapo juu mmetuwekea na lipicha lenye mwamvuli wa tigo hiyo inadhihirisha kuwa nyie mmeshindwa ata kununua mwamvuli tu...
internet yenu ni mbovu hadi najuta kusajili laini ya mtandao huu,....Mikocheni na Tabata...internet ni mwendo wa kobe kabisa
 
1. Mageuzi tunayoyaona hivi sasa kwenye matumizi ya mifumo ya kidigitali na kielektronik nchini yanatokana na uwepo wa miundombinu bora ya mawasiliano kutoka TTCL Corporation. Tunajivunia mafanikio haya.

2. TTCL Corporation imetoa mchango mkubwa katika kuchangia ukuaji wa sekta mbalimbali za maendeleo nchini. Hivi sasa tumefanikiwa kutoa huduma za mawasiliano kwa Vyuo Vikuu vya Elimu ya juu, Ofisi za Mabalozi, Taasisi za dini, Makampuni, Wateja wa Nje ya Tanzania, Mabenki, Taasisi za fedha, Taasisi za Serikali nk.

3. Ni lazima tujivunie mafanikio haya, tumeimarisha huduma zetu za simu za mkononi kwa kutumia teknolojia ya 2G, 3G na 4G nchi nzima ili kuhakikisha ubora wa huduma ya Intaneti na Sauti zinapatikana muda wote. Na tunaendelea kuboresha zaidi ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu. Mageuzi yanaendelea

4. Hii ni hatua kubwa zaidi katika kuongeza mvuto kwa wateja wetu, tumefanya mageuzi makubwa katika kuongeza mvuto wa Maduka yetu ya Huduma kwa Wateja ili kutoa wigo kwa wateja wetu kufurahia huduma zetu kwenye mandhari mazuri. Tembelea maduka yetu upate huduma bora na nzuri kutoka kwa wahudumu wenye weledi na bashasha wakati wote.

5. Tunawashukuru sana wateja wote mliojiunga na mtandao wetu wa TTCL Corporation, tunajivunia sana kuwa nanyi. Tunawahakikishia tutaendelea kutoa huduma bora na zenye kiwango ili kuongeza chachu katika ukuaji wa maendeleo ya Taifa letu.

Asanteni kwa kutuunga Mkono.
6. Tumeongeza mawakala wa kuuza Vocha za Muda wa maongezi kupitia mawakala wakubwa na wadogo. Pia tumeimarisha upatikanaji wa Vocha kupitia njia za kielektroniki ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu, hivi sasa unaweza nunua muda wa maongezi kupitia T-PESA, Mawakala wa Selcom, Mawakala wa Mobistock, Mawakala CRDB na NMB, kupitia mitandao mingine ya Simu, Wakala wa TPB, Cellulant nk

7. TTCL Corporation tuna haki ya kujivunia, tumeimarisha biashara, tumeboresha njia za mawasiliano na tumeongeza uwajibikaji ndani ya Shirika ambapo juhudi zimeleta mafanikio makubwa kwa kutoa GAWIO kiasi cha Shilingi Bilion 3.6/- (TZS) kwa serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na 2018/2019.

8. TTCL Corporation tumeshirikina kikamilifu katika kuhakikisha tunapeleka mawasiliano katika maeneo yote ambayo miradi ya ujenzi wa viwanda unaendelea nchini, tumepeleka mifumo ya mawasiliano yenye ubora ili kutoa fursa kwa wawekezaji katika sekta ya Viwanda kuwa na mazingira Rafiki ya mawasiliano. Kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara tumepeleka mawasiliano ya Data na Sauti kupitia miundombinu ya TTCL Corporation kwenye Ukanda maalumu wa uwekezaji {Export Processing Zone (EPZ) na Special Economic Zone(SEZ) nchini ili kuchochea maendeleo ya sekta hiyo.

9. Tumegusa kila Miradi mikubwa kwa kuwapa Mawasiliano bora ya Data na Sauti, tunatambua umuhimu wa miradi hii katika ukuaji wa maendeleo ya Taifa letu. Tumeshiriki kikamilifu katika kupeleka mawasiliano ya Data na Sauti katika Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Mwalimu Julius Nyerere.

10. Tumehakikisha Sekta ya Afya inakuwa na miundombinu bora ya mawasiliano, tumeshirikiana na Wizara ya Afya na Taasisi zake katika kuimarisha TIBA MTANDAO ambapo Hospitali kubwa na ndogo nchini zimeungwa kwenye miundombinu ya mawasiliano ya TTCL Corporation ambayo imefanikisha utoaji wa TIBA kupitia mtandao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…