James Hadley Chase
JF-Expert Member
- Mar 25, 2020
- 1,984
- 3,695
TTCL imezindua Minara sita ya Mawasiliano katika Wilaya ya Mlele mkoani Katavi ili kuimarisha huduma ya upatikanaji wa Mawasiliano kwa Wananchi.
Uzinduzi huo umefanywa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (Mb) ambaye pamoja na mambo mengine amesema Serikali imedhamiria kuimarisha huduma za Mawasiliano na TEHAMA katika maeneo ya mipakani na maeneo yasiyo na mvuto wa kubishana ili kuchochea fursa mbalimbali za kiuchumi na kuimarisha sekta ya elimu na afya kwa Wananchi.
Minara hiyo iliyojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itawanufaisha wakazi wa Kaulolo, Kamalampaka, Kafuru, Songambele na Ibelamafipa.
Akizungumza katika Uzinduzi huo Mbunge wa Jimbo la Mlele Mhe. Francis Kamwelwe eishukuru Serikali kupitia UCSAF kwakuliwezesha Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kujenga mnara katika kata ya Inyonga Jimbo la Mlele.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Mhandisi Peter Ulanga amesema ujenzi wa mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 11.47 hadi kukamilika, mbapo kati ya hizo TTCL imetoa kiasi cha shilingi bilioni 6.35 na UCSAF imetoa kiasi cha shilingi bilioni 5.15.
#RudiNyumbaniKumenoga