Ya nakubaliana na mtoa mada hapo juu kwamba TTCL inaweza ikawa inahujumiwa na watu waliopo ndani yake,
naamini hivi kwa sababu siku moja nikiwa Makambako Njombe kwa shughuli zangu,kwa masikio yangu nilimsikia jamaa mmoja ambaye ni fundi wa ttcl akilalamika kwamba internet switch imepigwa na radi kapiga simu makao makuu ili iletwe switch nyingine cha kushangaza jamaa wa makao makuu akamuuliza una shi ngapi nitume nyingine jamani hii inaingia akilini kweli ????
Kampuni ina nguz zipo chooni halafu ipewe jukumu hilo... Mi sielewi kabisa. Kama sehemu ya mtandao wake ipo choo unategemea nini? Hii nguzo ipo choo cha baa pale karibu na stendi ya Iringa mjiniWadau nimekuwa nikikumbana na adha mara nyingi katika mabenki,TRA na hata maofisini unaambiwa mtandao hakuna mara mtandao uko chini.Hii inasababisha usumbufu na upotevu mkubwa wa muda.Nimejiuliza hili kutokana na uhakika mkubwa tuliopewa wakati mkongo wa taifa ulipozinduliwa kuwa accessbility ya internet itaimarika lakini sasa imekuwa kinyume chake.What has gone wrong?mwenye info plse.!
Mimi naweza kuanza kuamini na kunyorosya maneno kuwa ttcl inahujumiwa na watu toka ndani na nie yake! Conspiracy and greedy...
Ila TTCL nao wana mapungufu yao pia pamoja na kupigwa vita na akina VODA AIRTEL NA TIGO PLUS ZANTEL
nani kasema kuwa TTCL ndio wanatakiwa kusimamia mitandao nchini?
wao ni incumbent au tuseme ndio wana own facilities lakini makampuni mengine wanatumia mitambo yao kutoa net sehemu zingine.
kila idara wako huru kuchagua watumie service provider yupi wa internet.
kwa vile TTCL wamelala na hawataki wao kutoa services kwenye maofisi ya serikali ili kujiongezea kipato ndio maana matatizo haya yanakuwapo.
waratibu wakuu kwa hili ni TCRA ambao nao wamelala usingizi wa pono. hakuna kinachoendelea.
wao ndio wanatakiwa kuhakikisha mwasiliano yote ya mitandao, tv,radio,cables nk yanaratibiwa na kuwafikia watumiaji bila mizengwe na ubora unaotakiwa,sheria zipo sina hakika kama wanazitumia.
hama.amia kampuni nyingine.Kwa siye tuliokuwa wadau wa internet tunapata tabu sana kila siku hakuna internet kama shirika limekufa mtuambie jamani msione aibu tuhamie pengine jamani hasa wafanya biashara wa internet cafe
Nashukuru kwa michango yenu ila bado hofu yangu ni kuwa tulipaswa kuwa na mabadiliko makubwa kimtandao baada ya fiber optic kuwepo otherwise naamini TTCL kama shirika mama imeshindwa kudeliver at optimum.Kila mtu ajiulize ni muda gani hupotea knye foleni bank au TRA kwa kuambiwa mtandao uko chini!au ni lugha mpya kuhalalisha uzembe kama vile mtu anapojibiwa kuwa jina (halijaingia knye compyuta)!tuendele kujadili.