Tu Wepesi Wa Kusahau Tulikotoka
Kwenye moja ya safari zangu nilimkuta kijana ( pichani) akitoka shuleni. Kichwani amebeba kifurushi cha unga wa mahindi. Miguuni amevaa makatambuga. Yawezekana kabisa aliambiwa; " Ukitoka shule pitia mashineni". Wengi wetu tumetoka katika mazingira hayo. Na ni wepesi sana wa kusahau tulikotoka.
Hii nyumba inanikumbusha mbali sana jamani wakuu huu Umasikini tuliokuwa nao utaondoka lini jamani? Umasikini wetu jamani ni kama Donda Kuu lisilopona eee jaman Ewe Mwenyeezi Mungu isaidie Nchi yetu tupatie Viongozi wanaowapenda Wanachi wake na kuwahurumia na kuwasaidia Twafa jamaniii Duhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh