Tuachane na makocha wa formation za kucopy na kupaste

shungurui

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2008
Posts
3,765
Reaction score
5,160
Japo mimi sio kocha na sijawahi kuwa kocha wa mpira lakini ifike mahali makocha waache formation za kucopy na kupaste.

Eti unatumia formation fulani ya mpira simply eti kwa sababu inatumiwa dunia nzima, yaani hata kama huna hao wachezaji wa kusuport iyo formation utalazimishia tu ili mradi timu yako nayo ionekanike inatumia formation inayotumiwa dunia nzima ni ujinga mtupu.

Na hata ukisajari watalazimisha kusajiri kufit hiyo formation ya dunia, kwangu mimi nauita ni ukocha wa kukariri, na ni ujinga mtupu.

na aina huu wa ukocha una wa gharimu sana wachezaji wengine hata kama ni wazuri lakini wanaonekana hawana thamani tena kwa sababu ya aina ya makocha wa kucopy na kupaste.

Leo kagere aliyekuwa mfungaji bora mara mbili mfululuzo anakuwa hana thamani tena wala hapangwi mara kwa mara kwa sababu ya makocha wa aina hii wa kucopy na kupaste formation kisa ni formation maarufu ni ujinga mtupu.

sasa kama ni mwendo wa kucopy na kupaste si bora tuwape makocha wazawa tena wako wengi ni wazuri tu wakipewa support kama wanavyopewa hao wazungu watafanya vizuri tu, .mfano kama, akina mexime, matola

cha msingi wawe wanapewa refresher course ya wiki kama mbili kila baada ya msimu kuisha ili wawe wanakuja kitu kipya kila msimu mpya unaponza.

sasa hili kwa club za simba, yanga, azamu hawawezj kushindwa, maana wazawa hawawezi kujipeleka wenyewe kwao gharama ni kubwa na kipato chao ni kidogo.

Sasa ukiwatizama hawa makocha wa kigeni sioni kipya kwao zaidi ya kucopy na kupaste formation na wasipopata matokeo wanakuja na hadithi eti wachezaji hawafit kwenye hizo information kwa hiyo waletewe wachezaji wanaofit kwenye hizo formatiom, na tena wanapewa support na wachambuzi wetu, sababu na wao wameshatekwa na ile hali ya formation za kucopy na kupaste.

Sasa msimu unaisha na msimu mpya unakaria kuanza, ushauri kwa timu ya simba na zingine ni wakati sasa kuamini wazawa, tena wapo wazuri kuliko hao mnao waleta wazungu, cha msingi kama nilivyosema wawe wanapewa refresher course,

narudia tena ni wakati wa kwenda na wazawa, wapo wazuri wengi tuache kukariri sasa kama nyie viongozi ni wazawa na mnafanya vizuri na mnaamiwa, sasa kwanini na nyinyi mnashindwa kuwaamini makocha wazawa? magori, kaduguda na wengineo mko vizuri sana, sasa ni wakati Kuangalia wazawa kama ni mgeni asiwe wa kucopy na kupaste formation wanaua moral ya wachezaji halafu mnasema hawajitumi, wachezaji za ni binadamu, makocha wazawa wapo wazuri tena kushinda hai mnaowaleta, na ninajua mnajua.
 
Bonge la point mzeya....hapa tulete tuu wakina matola na meky. Hamna sababu ya kuwa na makocha wakigeni ambao hawaleti faida kwetu.

Kwanza wazawa tukiwaamini na kuwaendeleza mbona watapiga kazi tuu. Tatizo la sie wafrika ni manyani huo ndio ukweli basi tuu tunakasirikaga wadhungu wakituambia ukweli. Wewe kwanza chan ilikuwa na sababu gani ya kwenda na ndariagije kama kocha mkuu wakati hiyo mdio ilikuwa platform mahususi ya kupromote makocha wazawa?

Sasa mbaya zaidi sio bongo tuu ata africa in general kuna huo upuuzi. Juzi ivory coast wamempa timu mzungu kibabu wa miaka 68 kuwa national tim coach. Cha kushangaza sasa ni kwamba kolo toure ambaye ni assitant kwa branden rogers pale leicester city mwenye uefa pro licence anaambiwa aapply kama assistant coach. Vichekesho hivi. Yaani unamtosa mzawa wakati qualifications anazo. Ndio hapa bongo wapo watu wana qualifications lakini tunaenda leta makocha toka burundi with similar qualifications....sii ujinga huo. Kinachoangaliwa hapo ni 10percent tuu hamna lingine.

South africa bennie mccarthy alikuwa in the running for the national team job. Wamemtosa wanampa kibabu cha miaka sabini...sasa unajiuliza hivi kweli sie waafrica tunashindwa kufikiri ata kidogo? Why yote hiyo ni roho mbaya tuliyokuwa nayo waafrica towards each other.

Tukija kwenye suala lako la mifumo ya copy and paste. Kwanza tuwe wakweli timu nyingi hizi kocha hafanyi usajili yeye kwa silimia mia moja. Mara nyingi makocha wanakuwa na prefered system of play yoa na hivyo atafanya usajiri wa wachezaji kwendana na mfumo huo. Hapa unakuta kocha anakuta wacheza na kusajiliwa pia without kujali yeye anapenda kucheza vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…