SoC04 Tuachane na matumizi ya vocha, tulipie intanert kama ambavyo tunalipia bili nyingine mwisho wa mwezi

SoC04 Tuachane na matumizi ya vocha, tulipie intanert kama ambavyo tunalipia bili nyingine mwisho wa mwezi

Tanzania Tuitakayo competition threads

MIKAEL MTANZANIA

New Member
Joined
May 28, 2024
Posts
3
Reaction score
2
Kwa mkono wa Mikael Mtanzania

Tanzania
ni moja ya nchi yenye gharama ndogo sana ya vifurushi vya internet kwani Gb 1 ambayo ni MB 1000 ya internet unaipata kwa elfu tatu ukweli ni jambo zuri na tunaweza kujipongeza kwa upungufu wa gharama hii.
lakini ukweli ni kwamba bado tunayoshida ya matumizi ya vifurushi vya intanert hasa kwenye makampuni ya mitandao ya simu kwa namna moja pesa inayotoka kununua kifurushi cha intanert wakati mwingine hailingani na matumizi ya mtu husika, ila kampuni za mitandao zikabuni kamfumo kakujikadilia ukitaka ununue kifurushi cha data cha mia tano ambayo ukitumia speed ya 5G ndani ya dakika mbili huna kifurushi cha intanert.

kitu kinachoumiza zaidi ni kuwa kifurushi hicho hicho ulichonunua unapewa muda wa kukitumia, kwangu mimi huu utaratibu hauko sawa pesa niliyo nunua kifurushi nakadiliwa muda wa kukitumia, na nisipoitumia ndani ya muda niliopewa inakatwa inamaana nimepoteza pesa yangu bila mimi kuifanyia chochote, hii haiko sawa kabisa pesa lazima ilipe gharama uliyoitumia na sio kuchukuliwa tu bila kuifanyia kazi yoyote.

Ningelitamani kuona huu mfumo wa vocha unatoweka kabisa ili tubaki na mfumo wa Routers, ambapo kuwepo na system maalumu itakayo piga hesabu ya matumizi ya kifurushi changu kwa mwezi halafu nilipie gharama, kama ambavyo nalipa gharama nyingine kwa mwezi, lakini mfumo huu uje na makadilio sahihi ya matumizi yangu ya intanert kwa mwezi, na sio kuniuzia vocha ya 5000 na muda ukisha nakatwa hapana, au uniuzie Routers uniambie kwa mwezi nilipe kihasi kadhaa, nitajuaje matumizi yangu kwa sababu kila mtu anayo matumizi yake ya intanert je kama nalipa pesa ndogo na matumizi yangu makubwa, au nalipa pesa kubwa na matumizi yangu madogo.

Nivyema matumizi ya vocha tukaachana nayo na tulipie intanert kama ambavyo tunalipa bili nyingine mwisho wa mwezi tena kwa mchanganuo mzuri unaoeleweka wa matumizi ya kila mmoja wetu.

Dunia ni kijiji hii itasaidia mtu kuwa na uhakika wa bando popote pale mtu atakapokuwa na hatoumiza kichwa kuweka pesa kwenye simu au kununua bando la kutosha ambalo atakatwa muda wake ukiisha, hivyo akiwa na uhakika wa kifurushi ambacho anaelewa mwisho wa mwezi itakuja bili yake atalipa.
Kwa dunia ya sasa huwezi ipishanisha intanert na maisha ya watu, kila jambo sasahivi kwa asilimia kubwa linapatikana mtandaoni, na lazima watu waingie mtandaoni kuona dunia inavyozunguka.

Hivyo lazima kuwe na uhuru wa matumizi ya Intanert kwa kila mtu wakati wowote muda wowote mahala popote, kwaiyo ni maoni yangu kuona tunaachana na haya mambo ya vocha na tulipie intanert kama ambavyo tunalipa bili nyingine mwisho wa mwezi.

Lakini ni vyema pia baadhi ya maeneo maalumu na makubwa pawe na free intanert mfano Hospitali hii isiwe kwa wafanyakazi tu wa hospitali iwe kwa watu wote ambao wameingia Hospitali, itasaidia watu kupashana taarifa kwa wakati.

Maeneo kama stend za mabasi kwani kukiwa na uhakika wa intanert sehemu yoyote pia utaweza kupata habari muda wowote hata ndugu zetu walioko vijijini huko itakuwa rahisi kuungana na dunia kwa ujumla,
lengo ni kuweka mfumo sahihi utakao saidia watu kupata intanert pasina wasiwasi lakini pia kuhakikisha mtu hapotezi pesa yake kukatwa bila mpangilio maalumu kwangu mimi ni vyema gharama za intanert zilipwe kama ambavyo zinalipwa bili nyingine.

Kwa hapa nyumbani Tanzania inafikilisha sana ukienda baadhi ya vyuo hakuna free intanert kabisa, na wakati wanafunzi wanahitajika kufanya tafiti mbalimbali mitandaoni, kama ni ngumu kuwa na hiyo free intanert basi naomba, tutumie njia hiyo niliyoisema hapo juu tulipie internet kutokana na matumizi ya mtu kwa mwezi na sio kuibiwa wazi wazi.

Mtu mmoja anweza kujiuliza je? kila mtu ataweza kulipa kwa huo mfumo kwani kuna wengine hawana ajira watamudu vipi hizo gharama za kulipia intanert kila mwezi, Naomba niweke sawa kukiwa na mfumo mzuri inawezekana kabisa, mbona maji tunalipa mwisho wa mwezi kutokana na matumizi ya mtu husika, mbona umeme tunalipa au tunatumia bure.

Kidogo naona kampuni za mitandao zimeanza kutoa Routers ili kuwaokoa watu wa maofisini, lakini bado gharama za Routers zipo juu kwa maisha ya mtanzania mmoja mmoja. Yes zipo juu ningependa kuona napigiwa hesabu kwamba mwezi huu umetumia MB kadhaa hivyo unahitajika kulipa, Mfano WhatsApp umetumia MB 20, Google MB 6. Instagram MB 30, Tik Tok MB 50, Twitter MB 5. Hivyo jumla umetumia MB kadhaa gharama yake ni kiashi cha shilingi kadhaa, inapaswa iwe hivyo unapewa mchanganuo vizuri kabisa wa matumizi yako na unalipa bila kinyongo wala dukuduku lolote moyoni.

Naamini Itamsaidia mtanzania hata asipokuwa na hela leo lakini bado anayo nafasi ya kutumia internet, najua wazi kabisa haya makampuni ya mitandao yakiweka njia nzuri za kulipia intanert kama ambavyo tunalipa gharama nyingine mwisho wa mwezi kwa mchanganuo mzuri, na kuhakikishieni Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa mno upande wa hiyo sekta kwenye hii dunia.

Ni yule mtibeli wa kisukuma
 
Upvote 2
kinachoumiza zaidi ni kuwa kifurushi hicho hicho ulichonunua unapewa muda wa kukitumia, kwangu mimi huu utaratibu hauko sawa pesa niliyo nunua kifurushi nakadiliwa muda wa kukitumia, na nisipoitumia ndani ya muda niliopewa inakatwa inamaana nimepoteza pesa yangu bila mimi kuifanyia chochote, hii haiko sawa kabisa pesa lazima ilipe gharama uliyoitumia na sio kuchukuliwa tu bila kuifanyia kazi yoyote.
Nakubali kwa kiwango fulani. Japo mitandao nayo inafanya kila mbinu kujiendesha kwa faida.

Lakini ni vyema pia baadhi ya maeneo maalumu na makubwa pawe na free intanert mfano Hospitali hii isiwe kwa wafanyakazi tu wa hospitali iwe kwa watu wote ambao wameingia Hospitali, itasaidia watu kupashana taarifa kwa wakati.
Kama walivyofanya uwanja wa ndege

Naamini Itamsaidia mtanzania hata asipokuwa na hela leo lakini bado anayo nafasi ya kutumia internet, najua wazi kabisa haya makampuni ya mitandao yakiweka njia nzuri za kulipia intanert kama ambavyo tunalipa gharama nyingine mwisho wa mwezi
Mtibeli umeeleza vizuri, japo hapo kwenye kulipia hiyo bili isiwe kama bili za maji za kutumiaaaa kisha ndio unalipia...... inabidi iwe kama bili za umeme: unajaza uniti na unatumia hadi zinapoisha kisha unajaza tena. Mfumo huu ni bira zaidi kwa pande zote mbili za makampuni na wananchi.

Lakini oia kuhusu free internet
hapa nyumbani Tanzania inafikilisha sana ukienda baadhi ya vyuo hakuna free intanert kabisa,
Tunaweza kulipatia hilo jukumu shirika la mawasiliano TTCL maana ndilo linalotumia kodi za wananchi.
Tena TTCL ndiyo inaweza kufungua milango kuanza na uuzaji wa mabando na vocha zisizokwisha muda wake ili kuonesha kwamba inawezekana na inayo faida. Na hata kama ni hasara tutaibeba wananchi wote kama ambavyo tumezibeba hasara zote zilizopita kupitia kodi zetu
 
Back
Top Bottom