Tuachane na Rais Magufuli tudai katiba mpya.

Tabutupu

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2010
Posts
13,206
Reaction score
18,549
Bila katiba mpya , hakuna uwezekano wa upinzani wala! ananchi kushinda dhidi ya ccm. Tatizo kubwa katiba ya sasa iliongezewa kipengere cha vyama vingi bila kuvunja vipengere vilivyo kua chini ya chama kimoja.

Mfano, Tume ya uchaguzi ilikua chini ya ccm pamoja na polisi tokea mwanzo walikua watiifu kwa chama cha mapinduzi.

Kwa hiyo mkurugenzi wa halmashauri kutangaza matokeo ya uchaguzi ni sawa na simba kumwona anacheza na nyumbu akiwa ameshiba, lakini akiwa na njaa ndio haya yaliyo tokea Jana kwenye chaguzi za madiwani.

Kwa maana hiii kwa sasa tuachane na magufuli, tudai katiba, hii iwe ndio agenda ya kwanza kwa watanzania wote na vyama vyote vya siasa hasa vyama vya upinzani.

Bila katiba mpya hakuna chama kitakacho shinda , wakiamua wanaweza shinda asilimia 100 kama walivyo Fanya Zanzibar.

Japo Africa ni kawaiada kuipotezea katiba. lakini walau tutakya na tume, mahakama na bunge vilivyo huru...

Katiba hii inaturudisha nyuma hata kimaendeleo, imepunguza utendaji, kwa sababu kila chombo kinasubiri maamuzi ya mqenyekiti wa ccm.

Mungu ibariki Tanzania.
Katiba kwanza , mengine baadae.
 
Tabutupu: Utatumia jukwaa gani au miujiza gani kudai katika katika utawala ambao umesema wazi kabisa kwamba katiba siyo kipaumbele chake?
 
Katiba mpya utaanza je? nasisi niwaoga kama nini huwezi kupata katiba mpya on a "slaverplate" sacriface ni lazima sasa nani iko tayari kulianzisha??
 
safi, tuanze hapa jamii forums , then Facebook, twitter, baadae mitaani , IPO siku watasikia. Hili ni jukumu LA kila mtanzania.

Maana hata huko ccm moto unawaka.
 
Katiba mpya utaanza je? nasisi niwaoga kama nini huwezi kupata katiba mpya on a "slaverplate" sacriface ni lazima sasa nani iko tayari kulianzisha??
Ni kuamua tuu , tukianza Leo inaweza chukua miaka kadha Ila kadri tunavyo chelewa ndio tunachelewesha ukombozi.

Hata biblia inasema, ukimdai sana mdeni wako IPO siku ataona ni karaha atakulipa japo kwa kuchelewa.

Muda wa kudai katiba ndio sasa
 
Africa mambo hayafanyui hivyo viongozi wa Africa hawanaga Aibu "in africa right is not given but is taken"
 
Kama unataka katiba mpya ili uje kushinda uchaguzi, utoipata hadi utakapokufa.
 
Bila katiba mpya , hakuna uwezekano wa upinzani wala! ananchi kushinda dhidi ya ccm. Tatizo kubwa katiba ya sasa iliongezewa kipengere cha vyama vingi bila kuvunja vipengere vilivyo kua chini ya chama kimoja.

Mfano, Tume ya uchaguzi ilikua chini ya ccm pamoja na polisi tokea mwanzo walikua watiifu kwa chama cha mapinduzi.

Kwa hiyo mkurugenzi wa halmashauri kutangaza matokeo ya uchaguzi ni sawa na simba kumwona anacheza na nyumbu akiwa ameshiba, lakini akiwa na njaa ndio haya yaliyo tokea Jana kwenye chaguzi za madiwani.

Kwa maana hiii kwa sasa tuachane na magufuli, tudai katiba, hii iwe ndio agenda ya kwanza kwa watanzania wote na vyama vyote vya siasa hasa vyama vya upinzani.

Bila katiba mpya hakuna chama kitakacho shinda , wakiamua wanaweza shinda asilimia 100 kama walivyo Fanya Zanzibar.

Japo Africa ni kawaiada kuipotezea katiba. lakini walau tutakya na tume, mahakama na bunge vilivyo huru...

Katiba hii inaturudisha nyuma hata kimaendeleo, imepunguza utendaji, kwa sababu kila chombo kinasubiri maamuzi ya mqenyekiti wa ccm.

Mungu ibariki Tanzania.
Katiba kwanza , mengine baadae.

Hlli ndilo tunapaswa kulibebea bango. Hakuliki hakulaliki tudai katiba mpya. Hakuna haja ya kushiriki kwenye chaguzi zozote. Njia ilikuwa hapa. Palipo na nia pana njia.
 
Back
Top Bottom