chibuOG
Senior Member
- Apr 11, 2024
- 169
- 337
Asalaam Aleikum Wanajukwaa,Natumai wote mko poa na mnaendelea na harakati za maisha ya kila siku.
Niende moja kwa moja kwenye pointi ya MSINGI ambayo ni Timu ya Taifa ya Tanzania yaani TAIFA STARS.Kama kichwa cha habari hapo kinavyojieleza kuwa tunatakiwa tufanye uwekezaji wa kweli kama tunataka mafanikio ya kweli kwenye soka letu,Kwa maana hizi lipua lipua na bahati nasibu haziwezi kutufikisha nchi ya Ahadi ya maziwa na Asali.
Cha kwanza, Ligi za vijana za under 17 na under 20 zisiwe mabonanza bali ziwe ligi haswa kama ilivyo ligi kuu.Yaani kama inawezekana ratiba ya ligi kuu ya NBC ndo iwe ratiba ya under 17 NA UNDER 20 vilevile ili kuwaandaa hao vijana kwaajili ya ushindani wa kweli.Huwezi kumuandaa kijana ambae anatarajiwa kucheza ligi kuu na timu ya Taifa kwa bonanza la wiki mbili au mwezi mmoja halafu awe tayari kucheza Ligi kuu.
Cha Pili,Mafanikio ya Vilabu vya SIMBA,YANGA na AZAM yasilipumbaze Taifa tukaona kuwa tumepiga hatua kubwa kisoka.Kuna gape kubwa mno la ubora na uwekezaji kati ya vilabu hivyo vitatu na vilabu vingine vya ligi kuu Tanzania.Kwahiyo tuweke mazingira sahihi na yenye usawa ili uwekezaji ufike mpaka huko kwenye timu za kati na timu za madaraja ya chini kabisa.
Cha Tatu, Tutoe siasa kabisa kwenye mpira wetu kwa maana unatumika kwa manufaa ya wanasiasa na wala sio kwaajili ya maendeleo ya mchezo wenyewe.Tuweke mifuo thabiti ya uendeshaji soka bila kuvipendelea hivi vilabu vya kurithi vya Kariakoo ambavyo kimsingi ni Mtaji mkubwa wa wanasiasa na vinatumika sana.
Cha Nne, TFF ambae kimsingi ndio mzazi na mlezi wa soka la nchi hii waweke msisitizo kwenye kanuni na taratibu walizoziweka kuhusu soka la vijana maana kwasasa kinachofanyika ni kama kiini macho na kujitekenya wenyewe.Under 20 na under 17 ni geresha tu na vilabu vimeanzisha kukidhi matakwa ya kikanuni tu wala hamna msisitizo wa hilo jambo kabisa kwa vilabu na hata TFF wenyewe.
Ongeza zingine mdau tuweze kujadili kulisaidia soka la nchi yetu.Ahsanteni kwa kunisoma na Nisameheni kwa makala ndefu.
NB:HIVI ULISHAWAHI KUJIULIZA KAMA MO DEWJI, GSM NA BAKHRESA WAKIAMUA KUACHANA NA SOKA LA NCHI HII TUTARUDI HATUA NGAPI NYUMA? TUWEKE MIFUMO SAHIHI ITAKAYOVUTIA UWEKEZAJI WA KWELI TUSITEGEMEE PESA ZA WATU MFUKONI BALI VILABU VIJIENDESHE VYENYEWE.