#COVID19 Tuache siasa, tukubali habari zote nzuri na mbaya kuhusu chanjo

#COVID19 Tuache siasa, tukubali habari zote nzuri na mbaya kuhusu chanjo

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Moja ya sababu kushinda Jambo lolote lile ni kukubali uhalisia wake.

Huwezi kushinda Jambo fulani bila kukubali uhalisia wake, bila kujua pande zote za shilingi na hii inatutesa sana nchi zetu hizi ambazo serikali inacontrol kila kitu.

Kulikua na habari leo katika vyombo vikubwa vya habari Kama Reuters, Bloomberg, bbc n.k kuhusu watu waliokufa baada ya kuchanjwa chanjo ya corona.

Hii habari Millard Ayo nae akai-report mchana, lakini sasa ameitoa hiyo habari kwa kuonekana kama anarudisha nyuma jitihada za watu kuchanjwa.

Cha kushangaza huko kwa wenzetu ambao ndio wanatengeneza hizo chanjo, vyombo vyao vya habari bado hiyo habari ipo.
Na Wala hakuna anayehangaika kutafuta vyombo vya habari wanaoreport madhara ya chanjo.

Huku kwetu kwa kujifanya tunajua sana corona na kujua sana hii chanjo tunapiga marufuku habari ambazo zinaonyesha kuna madhara.

Tuache siasa, tukubali habari yoyote. Ikiwa njema waacheni watu wareport na ikiwa mbaya waacheni pia watu wareport.
Tunataka kuficha habari mbaya ili tufaidike nini?

Screenshot_20211220-180737_1.jpg
Screenshot_20211220-141117_1.jpg
Screenshot_20211220-180235_1.jpg
 
Wazungu wanapanbana kuokoa maisha ya watu wao,huku kwetu wanapanbana kuchanja watu hata Kama watakufa ili chanjo ya mzungu iishe.
 
Na bado pia kuchanja ni hiyari ya mtu wazungu uwazi unawaweka huru!
 
Back
Top Bottom