Tuache Siasa/Zengwe kwenye michezo,.

Tuache Siasa/Zengwe kwenye michezo,.

Geffy

Senior Member
Joined
Feb 10, 2012
Posts
129
Reaction score
92
Habari ndugu, inabidi Tanzania tufike sehemu tuache longolongo kwenye swala zima la michezo, kila siku tunasikia kauli hizi zinazokera na kuchosha masikio ya watanzania wengi "Msimu huu Tanzania tumejiandaa vya kutosha ili kuleta ushindani".
Lakini kila tunapowakilishwa katika mashindano tofauti tofauti tunakiwa kichwa cha mwendawazimu....
Tukirudi nyumbani baada ya kuzaliloshwa katika michezo hiyo pia huwa tunakuwa na kauliz nyingine inayokera " Michezo ina matokeo matatu, kushinda, kishindwa na suluhu" Kauli inayonikera kuliko zote ni hiyo.
Inakera kuona hakuna la maana, hakuna muendelezo katika michezo na kuleta masihara katika kila jambo.

.... TANZANIA TUBADILIKE....
 
Tatizo linaanzia kwenyei ligi zetu, timu inafungwa uwanjani uwezo mdogo inadai point za mezani, inafika kipindi baadhi ya watu wanaita waandishi wa habari na tv za nchi 60 ili tu kudai point za mezani, ubovu wa timu ya taifa unatokana na ubovu wa virabu vyetu.

Siku tukiacha magumashi kwenye ligi zetu hata timu ya taifa itafanya vizuri ila tukiendelea na haya magumashi ya virabu ya kariakoo tutegemee kuendelea kunyolewa kwenye mashindano ya kimataifa.
 
Back
Top Bottom