HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,567
mie leo msomaji tu hapa, nipate maujuzi....nijue namna ya kung'ang'ania....loh....
Kuna wakati mpenzi anaambiwa kabisa na mwenzake kwamba hatakiwi, lakini yeye anasema, "tutabanana humu humu hatoki mtu hapa." Bila shaka hiki ni kichaa cha aina fulani. Mtu akishasema sikutaki, maana yake hakuna tena kinachoweza kuwaunganisha, yaani hisia za upendo. Kulazimisha kuishi na mtu asiyekutaka ni kujifanya mtumwa bila sababu. Inabidi tuamke na kuwa sisi kamili kabisa.
Kipipi hao wanaorudishwa ni kweli wapo ila mimi nasema wanakua hawana msimamo........huwezi kunirudisha kwenye nyumba ambayo nimeshachungulia kaburi wallaih nakwambia,kama na undugu ufeee!!!!Kuna wengine kila mara wanakula vichapo na kufungashiwa vifurushi lakini wanang'ang'ania tu......duh!! Yaani huwa nawaangalia mara mbili mbili nakosa jibu, ila nadhani na familia zetu zinachangia wajameni. Wanawake wengine wakiachika huwa wanarudishwa tena kwa waume zao!
Ah mtambuzi...some times hiyo kitu ni so hard kukubaliana nayo...si unajua moyo wa kupenda hauambiliki jambo