Tuache ushabiki, hali ya uchumi wa nchi ni mbaya sana kwa indicators zifuatazo

TEMILUGODA

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2012
Posts
1,389
Reaction score
285
Wanabodi napenda kuwashirikisheni katika suala au kero ya udhaifu wa serikali hii katika kukuza uchumi wa taifa.

1.Nimefuatilia vyuo vikuu vingi na kugundua zaidi ya wanachuo 3000 hawajapatiwa mikopo yao tangu vyuo vilipofunguliwa septemba/octoba 2012[hawa ni wale wenye mikopo tangu zamani].

2.Familia nyingi zinakosa milo miwili kwasiku si mitatu tena kama ilivyozoeleka

3.Sekta nyingi hazijaingiziwa fedha stahiki kama ilivyopangwa kwenye National budget na kupitishwa na Bunge[rejea taarifa za kamati za zinazo endelea].

4.Huduma za jamii zinazidi kudorora[chakula bei juu,maji shida,wanafunzi wengi shuleni ni watoro nk.]

5.Utegemezi wa wahisani[Donnor dependence]unakuwa kwa kasi pengine kuliko kipindi chochote kile tangu tupate uhuru wa bendera mwaka 1961[rejea ziara zote za Rais alizofanya tangu aingie madarakani].

6.Mpango wa kilimo kwanza unazungumzwa na kuthaminishwa kwa petty bourgeoisie[mabepari] si kwa lumpens[wakulima wadogo-rejea yaliyotokea dumila leo].

7.Rushwa inaongezeka kwa kasi na hivyo maadili katika jamii hasa wataalam[profesional ethics]yanashuka ama kupotea kwa kasi.

8.Kutoweka kwa uwazi katika uongozi au utawala[lack of transparance-rejea orders za wabunge,madiwani na wajumbe wa kamati za ccm wanazotoa kwa wakurugenzi katika kuwashughulikia watumishi wanaonekana hawako kambi moja hasa kada dhaifu na waoga ya walimu ref,sumbawanga,mwanza,lushoto-tanga nk]

Sasa kwa mujibu wa Karl Max"mwanafalsafa katika mabadiliko ya kijamii" mimi binafsi naona nilazima sacrifice itokee kwenye jamii ndio equality[usawa], sereosness[umakini katika utekelezaji], transparance [uwazi-jiulize je kuna taarifa iliyoshiba juu ya mauaji ya Arusha,morogoro, Iringa, Singida,dar,tarime,songea nk? Je kunataarifa ya kushiba juu ya mateso yaliyompata Dr.Ulimboka?

Nashauri bunge ndilo liwe la kwanza kusacrifice,MATHALANI,BUNGE LIWE NA UTARATIBU WA KUPITISHA BUDGET KWA UMAKINI ZAIDI BADALA YA MAIGIZO YA MAZOEA.
 
Una hoja inayotakiwa kujadiliwa hongera kutufungua macho kwa upeo haya ssmu bisheni

ni ukweli usiopingika kua kuna hoja ya msingi ya kujadiliwa hapa kuhusu mustakabali wetu sisi kama taifa na tunakoelekea.
 
Tunaweza kujadili kwa minajili kwamba tutake wabunge kuikosoa serikali kitaalamu zaidi kwa kuenesha njia za kukuza uchumi with reference eg.MWANAUCHUMI X anapendekeza njia 1,2,3,4.....n za kukuza uchumi.OTHERWISE TUTAENDELEA KUIGIZA TU.Kunaumuhimu wa kuungana kupigania uhuru kamili[political,economical and social independence] badalala ya huu uhuru wa bendera tulio nao sasa.DONNORS WENGI NI WASIFIAJI SANA WA DEPENDENCE PROGRAMMES ZA LESS DEVELOPED COUNTRIES,TZ FOR EXAMPLE KWA LENGO LA KUENDELEA KUZIKANDAMIZA KIUCHUMI.TUNAO UWEZO WA KUIGEUZA TANZANIA KIUCHUMI ENDAPO SISI WATANZANIA TUTAONGEZA UWEZO WA KUFIKIRI,UBUNIFU NA UWAZI JUU YA RASILIMALI WATU NA RASILIMALI GHAFI ZILIZOPO. Tuendelee kuchangia ili wabunge wetu wanaoingia humu wapate mawazo yetu yatakayo weza angalau kuwapa mwanga wa namna ya kugeuza hali ya uchumi wa taifa hili.JAMANI HALI YA UCHUMI NI MBAYA MNO MNO.
 
Bunge li-sacrifice??? Thubutuuuuuuu!!!!
 
Mkuu uko sahihi,mapaka leo serikali hii ya kishikaji haija ajiri walimu wapya. Inasemekana hali kiuchumi ni mbaya,ila mawaziri na viongozi serikali hutetea kwamba serikali ina fedha kumbe hamna kitu!
 
umeandika hoja nyingi za kufikirika kuliko uhalisia. Poor writing. wewe ni mwanafunzi wa mwaka wangapi? PSPA? kama uandishi ndo huu bora na huo mkopo wakunyime kabisa na si kukucheleweshea tu. kodi yangu inapotea bure kufundisha mtu kama wewe.
 
umeandika hoja nyingi za kufikirika kuliko uhalisia. Poor writing. wewe ni mwanafunzi wa mwaka wangapi? PSPA? kama uandishi ndo huu bora na huo mkopo wakunyime kabisa na si kukucheleweshea tu. kodi yangu inapotea bure kufundisha mtu kama wewe.

Wewe ni fisadi maana huwezi kusema hoja hizo ni kufirika wakati duniani bila kufikiri hakuna maendeleo,na mimi nakutwanga swali je,wewe mwenzangu ulisoma chuo kikuu enzi ipi? Maana unaonekana una-dependent thinking and claiming behaviour,hivi hujaona namna nilivyo weka hoja with evidance?NGOJA WAJE WAKUTWANGE,SI KILA AONGEAE KUHUSU MIKOPO YA WANAFUNZI NI MWANAFUNZI,BE A GREAT THINKER OF THE HITHERTHO!
 
Hali ya kiuchumi ni mbaya, lakini 93,000,000,000 za kujenga bomba la gesi zipo!! Huyu kikwete mpuuzi sana, mi nashndwa kuelewa anatengeneza filamu gani kwa script ya kipumbavu namna hii. Ndio maana naimiss sana MISIBA YA KITAIFA (bora wafe, hata kwa presha na kiharusi tu, JAPO TWAJUA UKIMWI NDO UNAOWAMALIZA, umalaya mtupu. Yamekalia kutafuta wanawake tisatisa kila nchi, wakati sisi hatuna matumaini. Ole wake atayeiba kura tena, ASHAKUM SI MATUSI
DAMU ITAMWAGIKA 2015,
Bora nife nikipigania future ya wanangu, kuliko waje kuishi kama ombaomba kwenye nchi yao
 

damu ya nani? acha uchochezi!
 
ila hapo ndo sijakuelewwa kwa nini useme hii ni kada dhaifu ???
 
kwahiyo ugreat thinker waku unakuaminisha kuwa kipindi hiki kimekosa transparance kuliko vipindi vya nyuma? unaweza kuleta evidence za hao zaidi ya wanafunzi 3000 ambao hawajaingiziwa mkopo? kwa kifupi ripoti yako ni ya kufikirika kama mwenyewe ulivyokiri. kumbuka ripoti haitakiwi kuwa yakufikirika bali uhalisia. ingekuwa ni uchambuzi hapo ningekubaliana na wewe.
 

Wewe usiwe mburura,au u mfanyakazi wa heslb? Kama unataka majina hayo pita vyuoni utapata,halafu nani kakuambia hiyo thread ni report?usijifanye msomi sana mbele ya wenzio,haki ninyi mnaopinga kila mawazo ya wenzenu kwa ujenzi wa taifa hili mna negative attitudes,na ndiyo maana nchi hii haiwezi kuendelea kamwe kwani nyinyi ndio wale mnaoamini kwamba matatizo ya nchi yameletwa na Mungu! KUBALI KWAMBA INDICATORS HIZO ZIPO,UCHUMI WA NCHI NI MBAYA MNO MNO MNO!
 

shida ni kwamba wapo watu wanaoweza kubisha tu hata kwa hoja zinaonekana waziwazi, sasa wewe unataka data gani au wewe upo nje ya maisha halisi ya kibongo? Wewe unaonaje mustakabali wa deni la taifa?, unafikiri ni kwanini serikali mpaka sasa haijaajiri waalimu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…