Uchaguzi 2020 Tuache utani, uchaguzi wa mwaka huu 2020 utakuwa mgumu sana kama Membe atagombea kupitia upinzani

Uchaguzi 2020 Tuache utani, uchaguzi wa mwaka huu 2020 utakuwa mgumu sana kama Membe atagombea kupitia upinzani

Lyaka Mlima Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2020
Posts
361
Reaction score
521
Kanda ya ziwa ni ya Magufuli Mwanza, Shinyanga, Kagera, Mara na Tabora na Simiyu.

Membe anachukua mikoa ya kusini ya walima korosho Lindi, Ruvuma, Mtwara, kwa msaada na nguvu ya Zitto Kabwe Membe atainyakua Kigoma.

Chadema watajitoa ktk kusimamisha mgombea, hivyo Membe ataichukua Kilimanjaro, Arusha kwa msaada wa Mbowe.

Kwa pemba , Tanga na unguja Maalim Seifu atamaliza game mapema kumsaidia Membe .

Kete kubwa itakuwa kuwin kura za Mbeya, Iringa, Morogoro, Singida, Dsm , Pwani, Rukwa, Katavi hizi ni kanda huru kwa kila mgombea.

Point of debate itakuwa suala la ajira kwa vijana wa chuo kikuu na wakulima wa mazao ya biashara.

Upande mwingine utanadi miradi yake.

Note. Udini, ukanda na ukabila kwa sasa ni jambo la kawaida
 
This game is over!
Msijiwekee fake hopes
 
Kama Udini na ukanda ni kawaida, jiwe anaweza kushinda maana kanda ya ziwa itambeba. Population ya kule si kidogo. Wale wanaweza wakachagua rais na sisi tukabaki tunatoa mimacho tu. Na kama mambo ya ukanda ni kawaida. Basi huwezi kuona kuna kanda zinaweza kugoma? Mfano inawezekana kabisa marais wakawa wanatokea huko tu kwasababu ya wingi wa wananchi wa huko.
 
Chadema haitairuhusu ACT isimamishe mgombea halafu wenyewe wawe wasindikizaji tu, haitatokea.
Hawana namna hao Chadema, hata makamanda uchwara waliozagaa hapa jamvini wameanza kumwangukia Zitto.
 
Lowasa hakushinda Uchaguzi ila alitoa changamoto kubwa toka mfumo wa vyama vingi uanze
Acha uongo. Kama unaongea hivi, basi kuna uwezekano mkubwa Lowassa alishinda. Membe yeye atafute mbinu ya kuzuia goli la mkono. Last time kazi ilifanywa na February Marope.
 
Naona kama wazipanga timu za mpira.

Uraisi wa Tanzania mpya ya sasa si kama kupokezana vijiti kwenye mbio fupi.
 
upinzani kushinda ni jambo moja na kupewa huo ushindi ni swala jingine

Hofu yako "labda" ina mantiki....

Lakini umesahau jambo moja, kuwa, MAJIRA na NYAKATI ndizo huamua matukio chini ya uso wa dunia.....

Majira na nyakati zikiruhusu, hakuna kinachoweza kuzuia GOLIATH asiangushwe chini na DAUDI tena kwa silaha dhaifu kabisa.....

Mkoloni mwingereza alikuwa na nguvu sana KIFEDHA na KIJESHI lakini kwa kuwa MAJIRA na NYAKATI havikuwa upande wao, waliachia Tanganyika mikononi mwa wazawa....

Vivyo hivyo ktk chaguzi hizi za sasa barani Afrika Tanzania ikiwemo, chochote chaweza kutokea...

Malawi juzi imetokea. Why not Tanzania?....Wait and see...
 
Kama Udini na ukanda ni kawaida, jiwe anaweza kushinda maana kanda ya ziwa itambeba.

Naishi moja ya mikoa iliyoko kanda ya ziwa Victoria. Mambo hayako kama mnavyofikiri...

Kanda ya Ziwa maana yake ni mikoa ya;
å Mwanza
å Kagera
å Geita
å Mara
å Simiyu
å Shinyanga

Kwa kabila Jiwe haieleweki ni kabila gani. Wengine wanasema msukuma, wengine wanasema ni jamii ya Warundi ama Wanyarwanda...

Shinyanga, Simiyu na Mwanza mainly ni kabila la jamii ya wasukuma. Si wote wanamkubali. Wengi tu wameumia chini ya utawala wake. Wengi wanaisoma namba. Hana uhakika wa kura zote. Lazima zigawanyike. Lazima ashawishi watu kwanini apewe muhula mwingine tens. Nasaba yake haina nafasi kwenye maisha ya watu...

Mara si mkoa wa wasukuma huo. Mainly ni Wakurya, Wajita na makabila mengine madogodogo. Huko kwa uhakika kabisa hana uhakikisho wa kura hata nusu tu. Kupata kura ni mpaka ajibu maswali ya kwanini anadhani anastahili apewe muhula mwingine. Lazima ashawishi watu kwa hoja na kutimizwa kwa ahadi zake mwaka 2015 vinginevyo hana kazi tena huyu. Hastahili muhula mwingine....

Kagera sio mkoa wa wasukuma. Huko wengi ni Wahaya. Hana nafasi katika mioyo ya wahaya. Hana uhakika wa kura japo ingalao kwa 50%. Anahitaji kushawishi watu ili wampe kura. Hatakwenda kuchukua kura kwenye kisahani....

Mkoa pekee anaoweza kupewa kura ingalao kwa 30% ni Geita nyumbani kwake. Kwingine kote huku kanda yq ziwa Victoria, anapaswa kushawishi watu na kujibu maswali na hoja za watu bila ya hiyana...
 
Hofu yako "labda" ina mantiki....

Lakini umesahau jambo moja, kuwa, MAJIRA na NYAKATI ndizo huamua matukio chini ya uso wa dunia.....

Majira na nyakati zikiruhusu, hakuna kinachoweza kuzuia GOLIATH asiangushwe chini na DAUDI tena kwa silaha dhaifu kabisa.....

Mkoloni mwingereza alikuwa na nguvu sana KIFEDHA na KIJESHI lakini kwa kuwa MAJIRA na NYAKATI havikuwa upande wao, waliachia Tanganyika mikononi mwa wazawa....

Vivyo hivyo ktk chaguzi hizi za sasa barani Afrika Tanzania ikiwemo, chochote chaweza kutokea...

Malawi juzi imetokea. Why not Tanzania?....Wait and see...
Well said comrade.
Ni suala tu la muda, dhulma, hujuma, na ukatili kwa watz unaotekelezwa na wenye mamlaka vitakoma, na hapo ndipo tutakapoanza kuwashughulikia kwa scale ambayo hata shetani atasikitika, mmoja baada ya mwingine,SASA BASI!!!
 
Membe ni mwepesi sana hajui siasa
Mtu mzito alikuwa Lowasa yule mzee itawachukua miaka 50 Wapinzani kupata tena kura kama zile

Lowassa alikuwa ni maiti hai kwenye siasa. Membe ana afya njema lakini hawezi siasa za ukweli, zaidi ya kutegemea mbeleko ya vyombo vya dola. Cdm nadhani walishapata funzo la kuokota taka ngumu toka ccm. Acha ACT waokote hilo jizee la ccm, lakini sioni lolote jipya. Tena Membe akichaguliwa na wapinzani ndio tutazidi kushusha idadi ya wapiga kura.
 
Siasa ingekuwa Rahisi hivyo, kila mtu angeweza kuwRais wa Nchi
 
Kamanda wewe huwa unatoa mtazamo wako, hii safi
Lowassa alikuwa ni maiti hai kwenye siasa. Membe ana afya njema lakini hawezi siasa za ukweli, zaidi ya kutegemea mbeleko ya vyombo vya dola. Cdm nadhani walishapata funzo la kuokota taka ngumu toka ccm. Acha ACT waokote hilo jizee la ccm, lakini sioni lolote jipya. Tena Membe alichaguliwa na wapinzani ndio tutazidi kushusha idadi ya wapiga kura.
 
Back
Top Bottom