MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Waungwana,
Hebu jamani tuache uharibifu wa lugha yetu maridhawa, Kiswahili. Ninayo mifano mingi ya uharibifu, lakini ngoja niwape hii michache.
1. Tangazo la Zain linasema "Ongea kwa Sh 1 masaa 24". Kwenye muda, hakuna uwingi, kwa hiyo, tangazo hilo lilipaswa kutamka "Ongea kwa Shs 1 kwa saa 24".
2. Watangazani wengi wa redio na luninga, na sasa hata vijana wengi, wanasema "nyimbo hii" wakiwa wanatamka juu ya "wimbo" mmoja. Tamko sahihi ni "wimbo huu". Ni Kiswahili potofu kutamka "nyimbo hii", kwani kwa usahihi, kinachopaswa kutamkwa ni "wimbo huu" au "nyimbo hizi".
3. Wanasiasa wengi huwa wanatamka "mashuleni" au "mahospitalini". Maneno "shule" na "hospitali" ni baadhi ya maneno ambayo hayana uwingi. Kwa hiyo, wanachopaswa kutamka ni "shuleni" au "hospitalini". Wengine wanadiriki kwenda mbali zaidi, na kutamka "maofisini", wakati walipaswa kutamka "ofisini", au "makazini" wakati walipaswa kutamka "kazini".
4. Kwenye hafla nyingi sana, watu hutamka "Kwa niaba yangu mimi mwenyewe..." Hii si sahihi hata kidogo. Huwezi kusema kitu kwa niaba yako mwenyewe... unasema kwa niaba ya mtu au watu wengine. Huwezi kujiwakilisha wakati wewe upo kwenye hafla hiyo. Neno "niaba" linatumika kwa kuwawakilisha watu ambao wapo au hawapo mahala unapokuwa unaongea; unaweza kuzungumza kwa niaba ya watu ambao kwa mujibu wa ratiba, hawawezi kuongea au itakuwa ni usumbufu, na pia, watu ambao kwa wakati huo hawapo mahala hapo.
5. Hili la mwisho ni baya zaidi, kwani linatumiwa na waandishi wengi wa habari. Mfano: "Binti huyo aliyetaka kubakwa aliokolewa na msamaria mwema..." Hivi hii inaingia akilini kweli? Kina mtu anayetaka kubakwa? Wangeandika: "Binti huyo aliyenusurika kubakwa aliokolewa na msamaria mwema..." ingeeleweka kwa usahihi wake. Lakini kwa kuwa siku hizi kwenye vyombo vya habari HAKUNA WAHARIRI, wanapitisha makosa ya AIBU kama hayo!
TUSIPOTOSHE kwa makusudi lugha yetu maridhawa, Kiswahili!
./Mwana wa Haki (Mwanafunzi wa Andanenga...)