Tuambiane! kwa nini uliamua kufanya biashara unayofanya sasa?

Joined
Jun 28, 2017
Posts
72
Reaction score
124
Habari wadau wa jukwaa letu pendwa la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali

Leo tuangalie na kuambiana(kuelezana)namna gani kila mmoja wetu aliefanikiwa au hajafanikiwa bado katika kufanya biashara au kutoa huduma anayotoa hadi sasa. Elezea japo kwa kifupi kwani huenda ikawa chachu na ukawasisimua “inspire” wengine kufanya biashara au kutoa huduma utoayo lakini kwa njia mbadala na bora zaidi

Kuna wengine waliingia katika biashara/ujasiriamali kwa sababu mbalimbali kama vile kwa sababu ya kukosa kazi au jambo kufanya kumshughulisha kupata kipato halali, wengine ni kutokana na kukosa ajira baada ya kusota mtaani kwa muda mrefu sana hivyo kuona njia mbadala ni kujiajiri kwa kuanza kufanya biashara au ujasiriamali na kuna wengine ni kutokana na asili ya familia au koo au makabila waliyotoka mfano kama Wachaga, Wakinga na Wayao (inavyoaminika wana asili ya biashara, makabila tajwa mniwie radhi ni mfano tu) na kadhalika

Kwa mleta mada nikiwa mchangiaji wa kwanza kwa ufupi tu sikuingia moja kwa moja katika biashara/ujasiriamali bali nilianza kwa kuajiriwa hadi kufikia kiwango cha SME Loan Officer Specialist katika taasisi ya fedha.

Baadae niliachana na kazi hii baada ya kugundua nina uwezo wa kusimamia mambo yangu baada ya kuanzisha ‘firm’ ambayo iliniasidia kuujua kwa undani zaidi biashara/ ujasiriamai kwa vitendo kwani nkupitia maandiko mbali mbali nikaanzisha miradi kama wa kuku wa kienyeji idadi elfu 4 na baadae biashara za mazao kuuza na kununua, biashara za usafirishaji (transit cargo)

Niliyojifunza na kuyaona ni kuwa biashara na ujasiriamali unahitaji kuwa na jitihada, nidhamu na juhudi za dhati kwa kila ufanyalo pasina kuhofu nini kitatokea (risks). Vile vile suala la aibu imekuwa mojawapo kati ya sababu za vijana wengi kutofanikiwa, kijana anaona aibu ataonekana mmachinga kutangaza bidhaa yake. Hii ni kwa kifupi sana lakini safari ni ndefu!!

Je nawe tuambie/tuelezee kwa nini wafanya biashara unayofanya leo?
karibuni
 
Nimefanya biashara zaidi ya 50 sasa sijui nianze na ipi!
Anza na 1. ulianzaje au nini hasa kilikuvuta katika biashara hiyo kwa kifupi 2. Unaifanya vipi biashara hiyo 3. Changamoto zake kwa kifupi 4. Kwa nini umedumu kwa muda mrefu katika biashara hiyo 5. Una nini cha kuwafundisha wafanyabiashara wachanga na jamii kwa ujumla!
 
Kwanza binafsi huwa sing'ang'anii biashara moja eti ili mradi nionekane nafanya biashara hiyo kwa muda mrefu bila kujali kama napata faida ama la!mfano siwezi kung'ang'ania biashara ya kuuza makoti wakati ni msimu wa joto kisa tu biashara yangu ni ya makoti!,kwa kifupi nimeanza kufanya biashara nikiwa na miaka 17 hadi Leo na nimefanya biashara nyingi kwanza kulingana na mtaji pili kulingana na mahitaji!mfano siwezi kufanya biashara ya bodaboda wakati mtaji wangu ni laki moja hata kama ndoto yangu ni kufanya biashara hiyo cha msingi nitaanza biashara yoyote inayoendana na mtaji huo hadi nifikishe kiwango cha Pesa nitachohitaji kwenye biashara ya ndoto yangu!nimesema nimefanya biashara nyingi lengo sio kubadilisha gia angani tu hapana Bali ni kufanya biashara kulingana na mtaji na mazingira nitakayokuwepo hadi nipate mtaji wakufanya biashara ya ndoto yangu!
 
Nipo ktk ujasiriamali kwa miaka 29, miaka 4 tu ndio nilifanya kazi ya kuajiriwa. Nitachangia point moja kati ya ulizotaja. Wengi hufikiria kujiajiri humweka mtu guru. Kujiajiri ni hukumu ya kifungo unachojihukumu mwenyewe(self imposed). Chagua shughuli au biashara kwa makini, usifuate mkumbo. Usiwe mwepesi wa kupata tamaa, tunza kumbukumbu za mapato na matumizi.
 
Kikubwa nilichojfunza kwenye kujiajir ni kupenda kile unachokifanya,
Pili Fanya kle ambacho unaexperiance au maarifa nacho.
Tatu kujifunza kumanage risk mana risk unavoidable ktk biashara.
Nne usimwamini mtu ukampa siri zako zote za biashara kirahisi rahisi..
Hayo machache tu ktk mengi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…