Tuambie kitu cha utundu sana ulichofanya utotoni na hutakisahau maisha yako yote

Tuambie kitu cha utundu sana ulichofanya utotoni na hutakisahau maisha yako yote

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Siku zote nakumbuka jambo moja la utundu sana nililofanya nikiwa mdogo ambalo sintakaa nilisahau. Ni kwamba kulikuwa na nyaya za umeme nje ya nyumba ambazo zilikuwa zimekatwa na ziko wazi, Na siku zote tulijua kwamba hizo nyaya zilikuwa na umeme, na nikawa wa kwanza kuwaambia watoto wenzangu wasiziguse.

Lakini sijui nilipata wazo gani pale ambapo nilitoa bamia yangu na kuamua kuzikojolea! Naambiwa kelele niliyopiga ilikuwa ya kutisha kama ya mnyama ambaye hajawahi kugunduliwa. Bila kutambua nilijikuta nimelala chini mbali na sehemu nilipokuwa nimesimama, ambapo bila kujitambua nilimalizia mkojo wangu kwenye kaptula!
 
Niliwahi kukuta jamaa kaopoa demu wake mahali wamejibanza gizani.
Kwa akili zangu za utoto nikawafuata nikawastua kwa sauti ya kustukiza ya ghafla.

Jamaa akadhani amebwambwa akatimua mbio na demu wake naye mbio.

Baada kama ya dakika mbili jamaa akatulia akaangalia akakuta ni dogo ndio nimemzingua, hakukuwa na hatari yoyote.

Jamaa akanifukuzia kwa machungu akakinikamata, alinipiga mtama enzi hizo tunaita ngwala, nikabinuka juu chini, nilivyotua hewani nikapoteza network kama dakika tano.

Yaani network zilikata nikashindwa kujua ni wapi nilikuwa nimetokea na ninaelekea wapi.
Jamaa kuona vile hofu ikamshika maana anilijua ni dogo wa kitaa, alikuwa ananifahamu, akataka kusepa kwa uoga kuwa huwenda ameniumiza .

Baada kama ya dakika tano hivi network zikarudi.
Nikaamka nikaelekea nyumbani.

Tangu siko hiyo adabu ilinishika, sijawahi mpaka leo kumzingua mtu nikimkuta yuko kichochoroni na mchepuko wake aiseee
 
Enzi hizo nipo maeneo ya shule ya mchikichini kwa wazee wa mapindi nilikua na sister angu binamu mmoja alikua na bahasha wake anauza viepe mtaa wa sikukuu basi ilikua kila siku namtimbia na mwanangu mmoja kua tumeagizwa viazi,,,jamaa alikua wa kuja full kujaza chips yai na kuku sometime hadi hela alikua anatoa maana alikua anajua vinaenda kwa dem wake kumbe ngoma vinaishia njiani..na simu zilikua hazipo jamaa alipataga tabu sana[emoji53] [emoji53] [emoji53]
 
Back
Top Bottom