Niliwahi kukuta jamaa kaopoa demu wake mahali wamejibanza gizani.
Kwa akili zangu za utoto nikawafuata nikawastua kwa sauti ya kustukiza ya ghafla.
Jamaa akadhani amebwambwa akatimua mbio na demu wake naye mbio.
Baada kama ya dakika mbili jamaa akatulia akaangalia akakuta ni dogo ndio nimemzingua, hakukuwa na hatari yoyote.
Jamaa akanifukuzia kwa machungu akakinikamata, alinipiga mtama enzi hizo tunaita ngwala, nikabinuka juu chini, nilivyotua hewani nikapoteza network kama dakika tano.
Yaani network zilikata nikashindwa kujua ni wapi nilikuwa nimetokea na ninaelekea wapi.
Jamaa kuona vile hofu ikamshika maana anilijua ni dogo wa kitaa, alikuwa ananifahamu, akataka kusepa kwa uoga kuwa huwenda ameniumiza .
Baada kama ya dakika tano hivi network zikarudi.
Nikaamka nikaelekea nyumbani.
Tangu siko hiyo adabu ilinishika, sijawahi mpaka leo kumzingua mtu nikimkuta yuko kichochoroni na mchepuko wake aiseee