Tuambie sababu inayokufanya usipumzike.....

Mwisho Wa Kazi Sio Mwanzo Wa Kupumzika, Ni Mwanzo Wa Kazi Nyingine

!
!
No Reforms No Election
 
Ndio maana mtu akifa tunasema pumzika kwa amani, sasa wewe unataka upumzike ukiwa mzima iweje
 
Ukipumzika vitu vinalala ni heri uchakarike kwa wiki siku 1 inatosha kabisa kutuliza akili
 
Binafsi naona ukiwa umejiajiri, una fursa kubwa ya kuweza kupumzika kuliko kuajiriwa

Ni suala la kusoma miamala tu ya mauzo kwenye simu yako, huku unakula zako upepo wa bahari
SIo Kwa biashara hii ya bongo aisee
 
ukipumzika kamari italala binti yangu

kupumzika ni kaburini
 
Kiasilia kila kiumbe akiwemo binadamu anapenda kuwa on top, independent and free..... ukiajiriwa kwa kiasi kikubwa unakosa hivi vitu

Ukianzisha banda lako la Chips ukaajiri na vijana watano wakusaidie kazi unaweza uka busy kweli kweli kuliko Mwalimu aliyeajiriwa
Utofauti wenu ni kwamba muuza chips ni Boss, anajitegema kufanya maamuzi na ana uhuru kufanya biashara atakavyo

Wakati mwalimu kiasili anajiona kama anapangiwa kila kitu kuanzia miongozo ya kazi na boss wake..... hayupo Top, hana maamuzi na hana uhuru

Hii ndio tofauti

Mentality mbaya kwa muuza chips ni ile akibweteka kwamba sipangiwa na akatumia muda huo kuwa mzembe biashara itakufa
Inatakiwa atumie “uhuru na uboss” wake vizuri kujisukuma zaidi kufanikisha jambo lake

Binadamu kawaida huwa anapenda sana kuwa kwenye confort zone...... mwili na nafsi zinapenda ku relax huku mambo yake yanaenda, lakini KIUHALISIA ili mambo yako yaende inahitajika juhudi kubwa ya kiakili na nguvu kufanikisha jambo lako liende ili ufanikiwe

Watu wengi wanapenda “kazi” ambazo hazina stress wala msoto lakini wawe wanaingiza mapesa mengi huku “wamepumzika”..... hii ni ndoto ya mchana

Mwana riadha Bolt aliwahi kusema watu wananiona nikiwa kwenye mashindano natumia chini ya sekunde 10 lakini naingiza mabilioni ya hela ila ukweli wasio ujua ni kwamba zaidi ya nusu ya muda wangu kwa siku moja natumia kufanya mazoezi, kufanya diet, ku train mind na mambo mengine mengi ambayo siku yangu naiona kama haitoshi

Mkuu sahau kabisa kuhusu KUPUMZIKA
Pumziko sahihi ni hakikisha angalau unalala masaa 6 kwa siku..... hili ni takwa la kibaiolojia

Siku ukijipata kwenye kamfereji ka hela za UHAKIKA kakifunguka nakuhakikishia kama itabidi hutawaza kabisa kupumzika
 
Hapo ni mpaka utengeneze mfumo mzuri wa kazi kujiendesha
 
SIo Kwa biashara hii ya bongo aisee
Jaribu kuweka mifumo ikusaidie kufanya usimamizi na uendeshaji wa biashara yako.

Kwa kufanya hivyo, utaweza kupata nafasi ya kupumzika japo Siku 21 Kwa Mwaka
 
Kupumzika ni most overrated statement...

Matajiri wenyewe hawapumziki, sembuse sisi ambao inabidi tutoke ndipo tupate milo ya siku?

Kupumzika literary ni kubadilisha activities tu, kiuhalisia hamna siku binadamu anapumzika na haipo recommended kiafya, mwili wa binadamu unatakiwa kuwa active muda wote na kuna ile biological therory ya use and disuse inayosema kwamba kiungo unachoacha kikitumia kinakua redundant na kinaanza kushrink uwezo wake, so muda wote akili na mwili vinatakiwa kuwa active ila kuchukua likizo ni kubadilisha ile routine yako kwa muda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…