MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,537
- 8,824
Tunaweza kubadili Familia zetu Mke/Mme/Watoto kupenda Kilimo na Ufugaji
Katika Maisha yetu ya sasa sio siri tuna kizazi kisicho penda sana kilimo wala kufuga,na walio oa wengi t mtakubaliana na mimi kwamba Wanawake/Wakina mama wengi sana wanapenda biashara za Saloon za Kike, Min Super Market, Duka la Nguo au la Vipodozi, Mwanamke yoyote lazima ataje hizo hapo biashara, Kijana alie maliza Chuo au shule yuko nyumbani ukimuuliza ni mradai gani umfungulie basi asipo taja Salooni ya Kiume, atataja Duka la nguo za vijana wenzake, au studio na kidogo sana Stationarie.
Ni ngumu sana kukuta Mama au Kijana anaulizwa project au biashara ya kufanya aseme anataka kilimo, au Ufugaji, hii kwa sasa hata vijana wa kijijini hawawezi taja kiimo wala ufugaji kamwe na ndo maana wakipata pesa kwenye kilimo wana kimbilia kwenye biashara za uchuuzi.
Sababu zinazo pelekea Wamama na watoto wetu kupenda aina hizo za biashara tajwa hapo juu ziko nyingi na chache ni kama vile;
Jamii zinazo wazunguka- Familia zetu nyingi zinazungukwa na watu wa aina gani? Marafiki za watoto wako ni wa aina gana? Wana fanya shughuri gani? Marafiki wakuu wao ni kichocheo sana cha aina ya kazi au biashara wanazo taka kufanya., kama mama marafiki zake yaani shoga zake ni wa mama wanao miliki Salooni, Maduka ya vipodozi na kadhalika basi Mama naye lazima atake hivyo vitu, the same kwa vijana.
Maisha yetu mengi asilimia zaidi ya 90 ni mjini-Maisha yetu mengi ni mjini tu hata kama tuna mashamba vijijini basi tunaendaga sana siku za mwisho wa juma tena sana kupiga picha na kuwalekekea vijana wa shamba dagaa na unga, kama familia yetu asilimia 90 ya maisha yao wako mjini ni vigumu sana kuja kuwashawishi waingie kwenye kilimo au wafuge, hawatakuelewa kabisa.
Kilimo na ufugaji kuonekana ni kigumu-Kilimo na ufugaji inaonekana ni kazi ngumu sana na inayo wafaa watu wa vijijini na ambao hawajaenda shule.
Taarifa hasi kuhusu Kilimo na Ufugaji-Ukiangalia hata kwenye vyombo vya habari asilimia kubwa ya taarifa za kilimo ni zile hasi, mara ukame, mara wadudu, mara wakulima wakosa soko la mazao yao, hizi taarifa huwatia sana uoga vijana.
Nini tufanye ili tuweze kubadili familia zetu wapende Kilimo na Ufugaji ili basi hata hatupo Duniani mashamba yetu yasije uzwa kwa saabu ya kuwa mapori;
Anzishia Familia mradi wa kilimo ulio tiyari kabisa- Kama ni Project ya kuku hakikisha project isha anza na kuku wanaanza kutaga na hapo wakabidhi wasimami, unapo wapa kitu kilicho anza kina wa motivate wao kuendelea kusimamia na pia pesa zinapo anza kuingia huona kumbe hii kitu ina pesa kuliko wanavyo sikia, hakikisha ni kilimo rahisi sana, hasa kilimo cha matunda na mboga mboga, unaweza funga green house kabisa, unapo wakabidhi shamba likiwa likiwa na miundo mbinu na pia likiwa na mazao yasio na ugumu inakuwa ni rahisi kwa wao kuendeleza, kuliko kuwakabidhi pori waanze kufyeka.
Shambani kwako Jenga nyumba ya kuishi- Hii ndo sababu kwa nini wazungu wanafanikiwa kwenye kilimo, make wanaishi mashambani kwao kabisa, sisi tunaishi mjini na tunaenda shambani mara moja kwa mwezi, kuwa na nyumba shambani kwako na ikiwa na kila kitu ni vizuri sana na wakati wa likizo familia nzima inaenda shambani, mnakaa shambani kule hata wiki mbili au moja, hii inawasaidia kuzoea maisha ya pale, unapo kuwa na shamba lako lina kuku, mbuzi na watoto wana enjoy supu za kuku na mbuzi na wanakula vitu asili kidogo wanavutika, kule nenda na vitu vyao vyote hadi mipira ya kuchezea na game zao, wakitoka shambani wana jiburudisha na game zao na kucheza mpira.
Usiwakabidhi mashamba ya mazao magumu- Mazao kama mahindi,Maharagwe, Mihogo, Mpunga au kilimo cha alzeti ni kilimo kigumu sana, kamwe usianze na aina hio ya kilimo kwao, wao sana waanze kulima vitu kama strawberry, nyanya,mboga za majani,kufuga ndege wa mapambo, wakianza na hivyo kwa baadae kuja kuwaambia waingie kwenye kilimo kikubwa itakuwa rahisi sana.
Kinacho fanya vijana na pia hata wa mama wachukie Kilimo na ufugaji ni kwa sababu ya aina ya kilimo na ufugaji tunao fanya, tunafanya ufugaji au kilimo ambacho kwanza mtu anaona ni kama adhabu vile, mfano unamwambia Watoto wako au Mke wako akawekeze kwenye kulima Mahindi au Alzeti, huko hatakubali, anza na vile rahisi na baadae anaweza kuja vutika huko kwenye mahindi, Alzeti na mihogo.
Tengeneza miundo mbinu yote kwanza- Usimwambie mtu asimamie kuku au kilimo bila ya kuwa umeweka miundo mbinu, na hakikisha miundo mbinu kama kuku ziko hatua yakutaga hapo unaye mwachia ataona inawezekana.
Wekeza kwenye kilimo au ufugaji wenye tija- Sio kila aina ya ufugaji au kilimo kina tija hapana jitahidi sana kuwekeza kule ambako kuna tija na hata unapo mwambia asimamie kweli anaona kuna tija make kuna baadhi ya ufugaji unaweza jikuta ni hasara badala ya faida na pia ni mateso, umeotesha mitiki unaambia asimamie hatakuelewa, au unalima vitu vigumu sana hawatakuelewa, unafuga Ng’ombe w kienyeji wanatoa nusu lita ya maziwa, hawawei kukuelewa kabisa.
Tofauti na hapo tujaindae siku hatupo Duniani baada ya miezi kadhaa familia ipige bei mashamba na mifugo make hivyo vitu kwao wanaona kama havina maana kabisa na pia hukuwahi hata kuwafanya wapende kile unacho fanya.
Kuna Mzee mmoja Mkoa mmoja wa Kaskazini, yule Mzee alikuwa na mashamba mawili makubwa sana moja hekari 600 na jingine hekari 1000, na mashamba yalikuwa na miundo mbinu yote kila kitu, Yule mzee alifariki mwaka 2018 na Familia yake haikuwa inapenda mambo ya shamba kabisa, hivyo shambani alikuwa anaenda mwenyewe na vijana wa kazi, watoto wake walikuwa ni wa mjini muda wote. Mzee baada ya kufariki ikabidi vikao vifanyike na zile mali yakiwemo mashamba wagawiwe, ninavyo andika walisha uza mashamba yote, wakauza trekita zote, wakauza combine harvester ya kuvuna ngano na pia mzee alikuwa na combine harvester ya kuvuna mahindi nayo wameza kwa kifupi wameuza kila kitu.
Tunaweza andaa familia zetu kupenda kilimo kuanzia sasa ili basi tunapo ondoka Duniani, zile idea zetu waziendeleze na pia kama sehemu yao ya ajira kutokana na ajira kuwa ngumu kwa sasa.

Upvote
2