SoC02 Tuandae wasimamizi wa kuendeleza Mawazo yetu mapema/Msimamizi wa biashara ya familia

SoC02 Tuandae wasimamizi wa kuendeleza Mawazo yetu mapema/Msimamizi wa biashara ya familia

Stories of Change - 2022 Competition

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2022
Posts
389
Reaction score
757
Moja ya vitu vinavyo tusumbua sisi ni swala zima la kuandaa Mrithi wa kusimamia mali pale ambapo Mungu anapo kuwa ametuita. Kwa watu kama wazungu au Wahindi hiki ni kitu cha kawaida kabisa kwao ambapo msimamizi wa baadae wa biashara za familia huandaliwa mapema sana na hii ni kwa sababu hakuna alie na guarantee na kifo.

Sisi mi kawada kama mzee mmoja kwenye crip moja alivyo sema, unakuta mimi nahangaika na Kilimo ila mtoto wangu yuko bise anatafuta kazi ya ualimu, au una Project ya Duka la vifaa vya ujenzi, ila watoto wote mmoja ni Mwalimu, mwingine ni muhasubu, sehemu Fulani na mwingine ni nesi na mwingine ndo anasaka kazi, maana yake nikiondo ndo basi.

Sisi mara nyingi sana Msimamizi wa Mali huchaguliwa baada ya Msiba ambapo familia hukaa kikao na kuteua watakao simamia mali au watakao ziendeleza bishara za marehemu, kwenye kikao kama familia ni kubwa huwa kuna mvutano wa hatari sana na mbaya zaidi ukute Marehemu alikuwa na wake wawili na wote wana watoto hapo ndo kuna kuwa na kazi ngumu sana ambayo saa zingine hubidi swala lipelekwe mahakamani. Angalia Mrema wa Impala, yule mzee alikuwa mjasirimali mkubwa sana kwa Arusha na kamwe hakuna asio mjua mzee Mrema, lakini angalia sasa baada ya yeye kuwa hayupo Duniani ni mwendo wa mivutano ya familia, na biashara zote zimefungwa na zingine kupigwa mnada, familia kila mmoja nataka chake, lakini kama mzee angeteua muendelezaji mapema na kumkabidhi kila kitu haya yasingetokea kabisa.

Madhala ya kuteua Wasimamizi wa family business mara baada ya muhusika kuwa hayupo ni makubwa sana na nitaainisha hapa;

Kutea msimamizi asie kuwa na uzoefu-Hii ndo tatizo kubwa kabisa ambapo unakuta kikao hukaa na kuanza kuteua wasimamizi wa mali za Marehemu, hapa huteuliwa asie kuwa na uzoefu na wapo ambao hufikia hata kuhonga wale wazee ili ateulwe yeye, na wengine huangalia tu kwamba huyu ndo mkubwa basi apewe na wengine huangalia labda elimu na kadhalika, Hapa huteuliwa mtu asie jua ABC za biashara za Marehemu na matokeo yake ni kuanza kusimamia ndivyo sivyo na mwisho wa siku hubakia Historia kwamba marehemu alikuwa na utajiri ila leo ni zero.

Kutea mtu mwenye malengo tofauti au mwenye hobby tofauti- Hili pia huwa ni kosa kubwa sana na hili nimeshuhudia mara nyingi sana ambapo Marehemu alikuwa ni mkulima na alie teuliwa hobby zake ni Biashara ya baa na kinacho tokea ni kuamua kupiga mnada mali za marehemu.

Kuteau mtu mwenye nia ovu- wapo wanao teuliwa lakini wakiwa na nia ambazo sio nzuri ambao hutokea kusumbua na kutesa sana familia, na mara nyingi anaweza teuliwa mtu ambaye ana malengo ya kulipiza visasi Fulani.

Kumbe tunaweza fanya vipi sasa kwenye kuteua wasimamizi wa Mawazo/Project za Marehemu? Maandalizi yanaeza anza mapema sana kwa msimamizi wa mali za familia;

Anza kuandaa msimamizi mapema sana akiwa angali mdogo ingawa unaweza usimwambia ila kwa vigezo vyako unaweza anza kumudaa mapema, na anaweza kuta ni ambaye unaona naendana na falsafa zako au ndo mkubwa kwenye familia au ndo wa mwisho au ndo wa jinsi fulani pekee.

Mpatie elimu ya kipekee, huyu hata elimu atakayo pewa inapaswa kuwa tofauti na wenzake, anahitaji elimu special sana hasa kama unamuandaa kusimamia miradi ya familia basi lazima elimu yake iendane na atakacho kuja kusimamia. Huyu hata shule hapaswi kusoma shule za mbali na wewe, usije mpeleka shule za Bording, anapaswa kuwa na wewe muda mwingi ili uweze kumfundisha mambo mengi hii wahindi wanaitumia sana.

Hakikisha una contro Marafiki zake-ni vizuri kujua marafiki zake ni wakina nani na wana tabia zipi ili basi msimamizi wako asije angukia mikononi mwa makundi mabaya, hii ni pamoja na rafiki zake wa jinsia tofauti, yaani rafiki wa kike au wa kiume wa msimamizi wako, ni vizuri kujua marafiki zake wote hao na mara nyingi wana mchango mkubwa pia.

Unapaswa kuwa una mpa mazoezi kwa vitendo sana, ya usimamzi wa miradi na hapa ndo swala la yeye kuto soma mbali na wewe linapo pata uzito, mazoezi ya kusimamia miradi yanapaswa kuanza akiwa mdogo kabisa hii itamjengea sana confidence na kujiamini na itampa uzeofu wa kutosha.

Penda sana kuwa unatoka naye mitoko mingi ya kibiashara na kuwa unamtambulisha kwa rafiki zako wa kibishara, hii itasaidia kuwajua mapema radiki zako na wao kuwa wanamjua ili hata siku haupo wawe tiyari walisha mjua na hawapati shida kuja kufanya naye biashara.

Unaweza mpatia baadhi ya Share au ukawagawanyisha wote share kama wako wengi na yeye akawa ndio mwenye share nyingi na utakuja kuwapa sababu za kwa nini yeye ana share nyingi kuliko wenzake, sana ni kwa sababu yeye ndo anasiamimia anatumia muda mwingi sana akiwa kwenye biashara. Kuwagawanyisha ni muhimu sana.

Kwenye kuandaa unaweza andaa moja au hata wawili au wote kulimngana na mipango yake na unaweza kuta una project tofauti tofauti hivyo ni bora basi kila mmoja akawa na project ya kusimamia.

Pia ni bora ukawa unapatiwa elimu nyingine hata nje ya elimu za biashara, hasa awe ni mtu sana wa Dini, maswala ya upendo kupenda watu mbali mbali, hii itakuja kumsaidia sana.

Kikubwa ni kwamba tusipo andaa Msimamizi wa kusimamia mali za familia mapema maana yake tutakuja kuwaachia mzigo mkubwa sana kutafuta msimamizi nahii itapelekea uhasama na hata kuuana kabisa. Familia inafika mahali hawa elewani na kesi ni nyingi mahakamani, kwa sababu tu ya Mali za marehemu na marehemu hakuacha mwongozo.

Na kamwe usifanye zima moto kwamba sasa unaona muda unaisha ndo unaita mmoja na kumuambia fulani wewe sasa nakukabidhi mikoba yote na simami, hii ni kosa sana kufanya zima moto kwenye kuandaa msimamizi wa mali za familia.

Wengi wetu najua tuna mifano mingi sana ya jijsi watu wengine ndugu, wengine marafiki wengine tunawajau tu ambao walikuwa na mali nyingi sana ila baada ya kufariki tu kila kitu kimeisha na sasa ni historia kwamba. Hakuna jambo jema kama hauko Duniani ila wazo lako linaendelezwa.

Aangalia wazungu, au hata wajapani, wahindi, wazazi wao walisha fariki miaka mingi ila mado mawzo yao yanaishi, idea zao zinaendelezwa, anagali TOYOTA, Sumsung, wakina Honda, angali wakina Ford, Dell na wengineo.

Karibuni kwa mawazo zaidi
 
Upvote 1
Mzee Mrema alimteua binti yake awe msimamizi wa biashara zote baada ya kufariki mashangazi wakawapamba watoto wa kiume mtakubalije mtoto wa kike awaongoze wakati nyie mpo hapo ndipo vita ilipoanzia
 
Back
Top Bottom