greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,653
- 3,060
MAKALA MAALUM
karibuni katika Makala nyingine yenye kuelimisha japo kwa uchache Juu ya mambo katika yaliyopo katika ujenzi.
Leo tutaangazia katika Mitindo/Styles za muonekano wa majengo.
1.Kama ilivyo kwa Mavazi na Simu;Majengo nayo huwa na muonekano wa mitindo tofauti tofauti yenye kuvutia.
-Wasanifu hutumia mda na ujuzi kwenye kuhakikisha Majengo huwa na muonekano wa kuvutia,yenye kwenda na nyakati husika.
2.Mitindo maarufu ya Majengo hapa Tanzania.
(Kwa wenye ukwasi)
i) Islamic Architecture
ii) Mediterranean Architecture
iii)Art Deco iv)Classical Architecture
(Kwa kipato cha kati)
v) Contemporary architecture
vi)Modern Architecture
vii) Swahili Architecture
viii) Mtindo wa Asili
3.MTINDO WA KI-ISLAM/ISLAMIC ARCHITECTURE
-Ulianza Karne ya 7,Pwani ya Ghuba ya Arabuni,umeenezwa na waarabu kipindi cha biashara za utumwa.
*Sifa za huu mtindo
- Una Msawazo:Mlango mkuu huwa kati,na upande wa kushoto utalingana na kulia.
- Paa za kulala paa zake uwa zina mgongo/angle ndogo sana na huwa zimejificha
- Uwepo wa Minaret:Hii ni minara inayojengwa kama sehem ya jengo
- Sehemu ya kati ya kupumzika na kujumuika
- Domes na Archs zilizochongoka
4.
Watanzania asili ya Uarabu huupenda sana nyumba zao ziwe na muonekano huu.
Mfano wa Islamic Architecture
-Ikulu ya Rais ya Dodoma na Dar
-Ikulu ya Rais wa Zanzibar
-Misikiti mingi ya Zanzibar na Bara
Ikulu ya Dar
5.MTINDO WA KIMEDITERRANIA-Ulianzia huko italia,Uhispani,Morocco,Ureno na Ugiriki, karne ya 16.
-Kwenye Tamthilia za Kihspania huonekana sana, nyumba kubwa zinazoitwa Hacienda
*Sifa zake
- paa za mgongoaa huwa za mgongo ulioinuka kidogo
- matilio za kufunika paa ni Vigae vya udongo
- Floor zake huwa ni marumaru za gharama
- Mbele ya nyumba huwa kuna bustani kubwa
- Rangi ya kuta itaendana na rangi udongo husika,mimea au maji
-kwa majengo ya Ghorofa moja au Mbili
-huu mtindo upo kwenye nyumba Masaki na Oysterbay
-Waarabu na wazungu huupenda sana
7.ART DECO
-Ulianzishwa 1920's huko Ufaransa
-Hapa Tanzania ulisambazwa miaka ya 1940's
*Sifa zake
- Kona za duara:kwenye makutano ya kuta hakuna pembe bali nusu duara
- Utumizi wa Rangi kali mf,Zambarau,nyekundu
- Urembo mwingi kwenye kuta zake
- Mlango kati,upande wa kushoto wa jengo ulingana na kulia.
-majengo ya makazi katika Kata za Kisutu,Kivukoni na Kariakoo
-Watanzania Wahindi wanaupenda sana huu mtindo.
9.MTINDO WA CLASSICAL
-Huu uhusisha mitindo ya Warumi na wagiriki
-ulianzishwa karne ya 4 BC
-Tanzania ulikuja kipindi baada ya uhuru
*Sifa zake
- Nguzo kubwa na ndefu sana na nguzo huwa kwa Idadi ya mbili mbili tu.
- Maumbo ya kijiometri
- Upangiliajo wa madirisha ,nguzo n.k hutegemea mfumo wa Golden section
- Sehemu ya nje ya kukaa watu e.g Patio,balcony
- Paa zake huwa na mgongo mdogoKida's plaza-mikocheni
-Ukitaka kumpa Architect tenda ya ku-designia kwa moja wapo ya mitindo hapo, lazima uhakikishe ana Ufaham vizuri
Mwisho wa sehemu ya kwanza
Nakaribisha maswali na maoni
Una shida yoyote kwenye ujenzi au jengo lako,na unahitaji ushauri...kuwa huru kunitafuta...
Utagharamika kwenye usafiri tu,
Ofa hii ni kwa mwezi April tu.