Tuangazie rushwa adui wa maendeleo

Mema Tanzania

Member
Joined
Feb 23, 2020
Posts
66
Reaction score
65
Tuangazie #Rushwa


Rushwa ni aina ya ukosefu wa uaminifu au kosa la jinai linalofanywa na mtu, taasisi, au shirika lililopewa madaraka, kujipatia faida haramu au kutumia nguvu vibaya kwa faida binafsi.


Rushwa inamaliza imani, inadhoofisha demokrasia, inakwamisha, maendeleo ya uchumi na inazidisha umaskini, mgawanyiko wa kijamii, kutokuwepo usawa na shida ya mazingira.


Kufichua rushwa na kuwawajibisha watoa na wala rushwa kunaweza kutokea tu ikiwa tunaelewa jinsi rushwa na ufisadi unavyofanya kazi na mifumo inayowezesha.


Misingi ya rushwa

- Rushwa inaweza kuwa ya aina nyingi, na inaweza kujumuisha tabia zifuatazo.

  1. Watumishi wa umma wanaodai au kuchukua pesa au upendeleo badala ya huduma.
  2. Wanasiasaa kutumia vibaya pesa za umma au kutoa kazi za umma au mikataba kwa wafadhili wao, marafiki na familia.
  3. Wanasiasa kuwahonga maofisa kupata mikataba yenye faida kubwa.


Rushwa inaweza kutokea mahali popote katika biashara, serikali, mahakama, vyombo vya habari, asasi za kiraia na sekta zote kuanzia afya, elimu hadi miundombinu na michezo.


Rushwa inaweza kuhusisha mtu yeyote: wanasiasa, maafisa wa serikali, wafanyakazi wa umma, wafanyabiashara au wananchi.


Rushwa na ufisadi hufanyika katika vivuli, mara nyingi kwa msaada wa wataalamu wa uwezeshaji kama mabenki, wanasheria, wahasibu, mifumo ya kifedha na kampuni zisizojulikana zinazoruhusu kushamiri kwa mafisadi na kuficha utajiri wao.


Rushwa huendana na mazingira yanayobadilika. Inaweza kubadilika kwa kujibu mabadiliko ya kanuni, sheria na hata teknolojia.


Athari za rushwa

Kisiasa | Uhuru wa muhusika na utawala wa sheria.​
Kijamii | Ushiriki wako na hata imani yako kwa serikali.​
Kimazingira | Nafasi yako ya mazingira mazuri na mustakbali endelevu.​
Kiuchumi | Nafasi yako ya kujenga na kukuza utajiri.​


#MemaAgainstCorruption

Tufuate kupitia Facebook, Twitter, Instagram na Medium - Mema Tanzania www.linkr.ee/mematanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…