Tuanze kujadili katiba ya Tanzania bara (TANGANYIKA)

Tuanze kujadili katiba ya Tanzania bara (TANGANYIKA)

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Kutokana na rasmu ya katiba ya muungano kuja na pendekezo la kuanzishwa serikari ya Tanzania bara na wazo hilo kuonekana kuungwa mkono na watu wengi sana na kuoneka kama limeshakubalika basi ni muda muhafaka kurijadili kwa kupendekeza muundo wake.

Kwanza napendekeza haya kwani utakuwa umebaki muda mfupi sana baada ya katiba ya muungano kukamilika hadi kufikia uchaguzi mkuu.
Katiba hiyo lazima iwe kamili kabla ya july 2015 ili itumike kwenye uchaguzi mkuu 2015.

Pendekezo langu kusiwe na wabunge ila kuwe na balaza la wenyeviti wa halmasauri.
Yani kila wilaya iwe na mwenyekiti wa halmashauri atakaechaguliwa na wananchi pamoja na majukumu ya kusimamia halmashauri husika, kufuatilia miradi ya maendeleo pia ndio awe mwakilishi wa wananchi katika baraza hilo. Hii itawafanya wenyeviti wawajibike zaidi na kuwafanya wananchi wawe na mtu mmoja anaowasemea na kuomba miradi ndie anayewasimamia.
 
ile ile tuliyokuwa nayo kabla ya muungano na Zanzibar (1961 - 1964), imwage hapa tuanze editing....
 
Rasilimali zote zilizobinafsishwa kifisadi zitaifishwe na biashara kati ya Tanganyika na Zanzibar iwekwe wazi,wazanzibar walipie umeme,chakula kifuate process za export,Zanzibar ichangie pesa kulingana na viongozi wao,mfano kama wana wabunge 20 wawagharamie wao sio Tanganyika iwafanyie wao waendeleze ubwanyenye wao
 
kwa maoni yangu ni mapema sana kuijadili katiba ya Tanganyika kabla hata hii rasimu hatujaielewa vema na kuiboresha kwanza.

Kumbuka hadi tufikikie hiyo ya tanganyika tuna safari tatu hatujafika 1. mapendekezo ya mabaraza ya katiba ngazi ya kata na wilaya 2. Mapendekezo ya Bunge maalum la katiba 3. Maoni ya wananchi kupitia upigaji kura.

hatuwezi kuanza kuijadili katiba ya tanganyika wakati hatujui wananchi watasema nini katika kura za maoni.
 
Hebu tuache tukokotoe rasimu kwanza,

wajumbe wa katiba wamechukua takribani mwaka kutufikisha hapa, siamini kwamba sisi wasomaji tunaweza kuchukua siku 5 tu kupitia mapendekezo yao, tukayaelewa na kuboresha.

kama ni dereva basi unaendesha gari kwa mwendo kasi wa ajabu aghalabu utatuua abiria wote hata tusifike tuendako.
 
Hebu tuache tukokotoe rasimu kwanza,

wajumbe wa katiba wamechukua takribani mwaka kutufikisha hapa, siamini kwamba sisi wasomaji tunaweza kuchukua siku 5 tu kupitia mapendekezo yao, tukayaelewa na kuboresha.

kama ni dereva basi unaendesha gari kwa mwendo kasi wa ajabu aghalabu utatuua abiria wote hata tusifike tuendako.
haya mambo ya rasimu, bunge la katiba nk huwa ni justification tu; katiba inaandikwa na system
 
Kujadili katiba yetu Watanganyika rahisi sana. Rasimu uliopo unatosha kuupitia haraka, na kuondoa yale ya Muungano, yanayobaki ni yetu. Yale ya Muungano tu yanaweza kujadiliwa kimtazamo wa Tanganyika. Natamani kuiona Tanganyika yetu ikirudi. Tumechoswa kuonewa kubebeshwa mzigo usiobebeka.. afu wanalia. Mtoto ukimbeba mgongoni afu analia bila sababu, basi ni kumweka chini atembee kama ndo anachotaka.
 
Rasilimali zote zilizobinafsishwa kifisadi zitaifishwe na biashara kati ya Tanganyika na Zanzibar iwekwe wazi,wazanzibar walipie umeme,chakula kifuate process za export,Zanzibar ichangie pesa kulingana na viongozi wao,mfano kama wana wabunge 20 wawagharamie wao sio Tanganyika iwafanyie wao waendeleze ubwanyenye wao

Hizo ni fikira mgando alikwambia nani z'bar hawalipi umeme au unamawazo ya kijiweni na hapa z'bar imeingia vipi ktk katiba ya tanganyika chuki zako kwa z'bar zitakuuwa maana huzidishi hupunguzi.
 
(Hizo ni fikira mgando alikwambia nani z'bar hawalipi umeme au unamawazo ya kijiweni na hapa z'bar imeingia vipi ktk katiba ya tanganyika chuki zako kwa z'bar zitakuuwa maana huzidishi hupunguzi.)

Truth hurts, To the best of my knowledge(fikira mgando) i under rate Zanzibar nation as parasite to Tanganyika,and to much talk talk for nothing.🙂
🙂🙂🙂🙂🙂We must remove all deasease from our new Born country
 
Hoja nzur sn ndugu....Kinachonishangaza ni aina ya usingizi tuliolala Watanganyika....usingizi ambao hata baada ya kuamshwa na ndugu zetu Wazanzibar walipokuja na katiba yao lakini bado tumeendelea kulala bila kudai ya Tanganyika...inakuja hii ya sasa ya Shirikisho lakini bado viongozi wetu si CCM si UPINZANI wanaamsha huu mjadala mpaka hoja ya msingi km hii inaishia kujadiliwa tu hapa JF....inasikitisha...
 
Tanganyika bila ya z'br inawezekana.
 
Guys, c kumkomoa mzanzibar wala mbara bali ni kwa maendeleo yetu sisi na Tz yetu... Mi nazani serikali tatu haifai kabisa...!!! Umeshindwa kutumoja na mbil, je utaweza hiyo tatu??

This page is for G/ thinkers.. So plz
 
We lengivaje sisi wazanzibar hatumtegemei mtu sisi yumefilisika kwa sababu ya muungano mbona hamujai hewa kila siku wazenji wanataka.kujitenga na nyinyi ila mnakua wagumu jua muungano unawafaidisha coz nyinyi ni tanganyika mulovaa mwavuli wa tanzania wezi wakubwa sisi hatutoi bidhaa hapo tu hata vutunguu tunatoa nje wakati singida vipo na tunatoa saruji nje wakati tanga ipo msitutishe nyinyi woga wa maisha
 
Tutengeneze Katiba ya Tanganyika kwanza ndio tutengeneze katiba ya shirikisho.... ili watanganyika tuulizwe tunataka shirikisho au la... coz zanzibar wao wanayo katiba yao..Tusibuluzwe Watanganyika...
 
Wa kulaumiwa hapa ni mfumo wa elimu yetu...hakuna mahali popote kwenye elimu ya uraia panapoelimisha umuhim wa muungano na ni maeneo yapi tumeungana kwa manufaa yepi...Lakini kimsingi ipo faida ktk muungano ni nyingi kuliko hasara....
 
Back
Top Bottom