Uncle Araali
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 950
- 1,262
Kwa muda mrefu,pamekuwa na jitihada na mashinikizo kutoka kwa vyama vya siasa,asasi za kiraia na wananchi wenye mapenzi mema na taifa lao la Tanzania.Harakati zote hii zimechochewa na jinsi katiba iliyopo ilivyo na walakini na dosari anuwai,ambazo wengi wanaona ni bora tuwe na katiba inayoendana na wakati huu,katiba inayowawajibisha viongozi wetu kwa maslahi ya taifa na kulinda haki na uhuru wa raia.Hili ni jambo jema kabisa.
Lakini kwa mtazamo wangu,tukiidai katiba mpya bila ya kutengeneza uelewa wa kisiasa kwa wananchi walio wengi,bado tutabaki hapahapa,licha ya kupata katiba mpya.Wananchi wengi bado wana uelewa mdogo na masuala mapana,hata yanayowagusa moja kwa moja.Hawajui kuwa kiongozi anapaswa kuwajibishwa,pale anapokwenda ndivyo sivyo.
Ninashauri kuwa,kwa sasa nguvu kubwa zaidi,pamoja na vuguvugu la kudai katiba mpya,vyama vya siasa,asasi za kiraia na raia wenye mapenzi mema wawekeze zaidi katika uelimishaji wa jamii kuhusu masuala ya kisiasa. Nawanukuu wataalamu wafuatao wa maswala ya siasa:
"Institutions alone are not enough to rein in elected autocrats. Constitutions must be defended - by political parties and organized citizens, but also by democratic norms. Without robust norms, constitutional checks and balances do not serve as the bulwarks of democracy we imagine them to be.
nstitutions become political weapons, wielded forcefully by those who control them against those who do not. This is how elected autocrats subvert democracy - packing and "weaponizing" the courts and other neutral agencies, buying off the media and private sector (or bullying them into silence) and rewriting the rules of politics to tilt the playing field against opponents"
(Steven Levitsky & Daniel Ziblatt: HOW DEMOCRACIES DIE)
Nawasilisha hoja.