Tuanze Upya kwa Kufuta Ushindani wa Vyama vya Kisiasa

Tuanze Upya kwa Kufuta Ushindani wa Vyama vya Kisiasa

uavyama

New Member
Joined
Aug 13, 2013
Posts
1
Reaction score
0
Mawazo haya yanatokana na imani kwamba Tanzania, nchi iliojaa neema ya kila hali, ingepata kada ya viongozi madhubuti wenye uchungu na Taifa, ingeweza kufanya mabadiko ya haraka na kutokomeza umasikini, magonjwa na elimu duni. Kikwazo kimoja kikubwa cha kupatikana kwa viongozi wa kaliba hiyo ni ushabiki na ushindani wa vyama vya siasa. Historia inaonyesha kwamba demokrasia ya vyama vingi Afrika haijasaidia kumtoa Mwaafrika kutoka kwenye maisha duni baadala yake sehemu nyingi imeleta machafuko, rushwa na ufisadi.

Ninaamini kwamba waafrika hatuko tayari kwa demokrasia ya ushindani wa vyama vya kisiasa kwani hatuna utamaduni wa ushindani wa itikadi. Pamoja na hayo maendeleo ya kisayansi, kiuchumi na kijamii dunuiani yamepunguza sana tofauti za itikadi. Kwa kiwango kikubwa leo China na Marekani wanazungumza lugha moja na wana ushirikiano mkubwa.

Tuanze upya kwa kujenga demokrasi ambayo wakati wote itatupatia viongozi wa hadhi ya kitaifa na kimataifa, viongozi safi walio tayari kujitoa muhanga kwa faida ya taifa. Amini usiamini viongozi hao wapo miongoni mwetu na watapatikana kama vikwazo vya kisiasa vikiondolewa. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema kwamba maendeleo yanahitaji vitu muhimu vinne; watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora. Watu na ardhi tunavyo kwa wingi sana. Ninaamini kwamba siasa safi na uongozi bora haviwezi kupatikana katika mfumo wa sasa wa ushindani wa vyama vya kisiasa.

Inawezekana kuwa na demokrasia bila ya vyama vya kisiasa. Demokrasi ni mfumo wa utawala ambao wananchi wanaendesha dola kupitia kwa wawakilishi wao waliowachagua. Historia inaonyesha kwamba utawala wa demokrasia ulianza Ugiriki karne sita kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo wakati vyama vya siasa vilianza kujitokeza karne ya kumi na nane huko Marekani. Kwa desturi chama cha siasa huundwa kwa nia ya kuchukua dola ili kutekeleza itikadi yake. Kinadharia itikadi ya chama ni kwa ajili ya manufaa ya taifa zima lakini uzoefu unaonyesha kwamba maslahi ya chama huwa ni muhimu zaidi.
 
Back
Top Bottom